NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
Hayo yamebainishwa leo Disemba 3, 2024 Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Oran Njeza wakati wa Mafunzo kwa Kamati hiyo yenye lengo la kuwajengea uelewa kuhusiana na mifumo ya ukusanyaji mapato wa TRA.
Mhe. Njeza amesema TRA wakiendelea kuwekeza zaidi kwenye mifumo ya ukusanyaji wa mapato itasaidia kuongezeka zaidi kwa mapato na Serikali itakuwa na mapato ya kutosha
Aidha Kamati hiyo imeishauri TRA kuwekeza zaidi kwenye TEHAMA ili kuhakikisha asilimia 50 ya bajeti inachangiwa na kodi za watanzania.
“Uboreshaji wa mifumo ya TEHAMA ufanisi katika ukusanyaji wa mapato na kuondokana na usumbufu na changamoto ndogondogo ambazo zimekuwa zikijitokeza”. Amesema Mhe. Njeza.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha Hamad Chande amesema serikali imeendelea kuimarisha mifumo ya ukusanyaji kodi na tayari imeshatenga bajeti kwaajili ya kuimarisha na kuboresha mifumo ambapo matokeo chanya yanaonekana ikiwa mwezi uliopita TRA kupitia mifumo hiyo ukusanyaji wa mapato umekuwa mkubwa kutoka bilioni 850 hadi kufika trilioni 1.2.
Nae Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda amesema wataendelea kutoa elimu ya mlipa kodi na kueleza kuwa hawatosita kuwachukukia hatua za kisheria wanaotoa risiti bandia na wanajihusisha na vitendo vingine vya kijinai.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge kuwajengea uelewa kuhusiana na mifumo ya ukusanyaji mapato wa TRA. Ufunguzi wa Mafunzo hayo umefanyika leo Disemba 3, 2024 Jijini Dar es Salaam.