Mtoto amwagiwa Petroli na kuchomwa moto kisa kuiba 800

Mtoto anayesoma Darasa la Tatu katika shule ya Msingi Kasota (9) Mkazi wa kijiji cha kasota Kata ya Bugulula Halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani humo amejeruhiwa kwa kumwagiwa mafuta ya Petrol na kuwashiwa moto sehemu mbalimbali za mwili wake na Mama yake Mzazi kwa kosa la kuiba Pesa.

Akizungumza na Millardayo Siwema Kulwa ambaye ni Mama Mdogo wa Mtoto huyo amesema chanzo cha awali mtoto huyo anatuhumiwa kuiba pesa ya mama yake kiasi cha shilingi 800 ndipo mama yake alipochukua uwamuzi wa kutenda tukio hilo la kinyama.

” Nilipigiwa simu nikiwa Geita na Majirani nikaambiwa Dada wahi hapa kwa dada ako kuna tukio nikauliza tukio gani nikaambiwa Dada ako kachoma mtoto moto nikauliza kisa nini akasema kisa mtoto kaiba 800 nikasema maana dada angu huwa ana matatizo ya akili , ” Mama Mdogo Swema Kulwa.

Mganga Mfawidhi kutoka Hospitali ya Wilaya Nzera Dkt.Shadrack Omega amekiri kupokea Mtoto huyo ambaye alikuwa amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kusema mtoto huyo anaendelea kupatiwa matibabu huku akisema mtoto huyo amemwagiwa mafuta ya petrol na kuchomwa moto .

Jitihada za kulitafta Jeshi la Polisi Mkoani Geita zinaendelea ambapo Mama Mzazi wa mtoto huyo anatuhumiwa kushikiliwa na Jeshi la polisi.

Related Posts