Na Pamela Mollel,Arusha
Riadha za TanFOAM Arusha zimetajwa kuwa kivutio kikubwa hususani kwa wakazi na Wageni mbalimbali waliopo katika jiji la Arusha
Pia mbio hizo zinatajwa kuwa za kipekee kutokana na ubora wa maandalizi mazuri zikiwemo zawadi nono kwa washindi ambazo ni fedha pamoja na magodoro
Aidha katika mbio hizo wanariadhaJoseph Panga na Hamoida Nassoro wamefanikiwa kuibuka washindi katika Mbio za riadha za TanFOAM Marathon zilizofanyika jijini Arusha.
Joseph Panga kutoka klabu ya JWTZ alifanikiwa kung’ara kwa kushinda kilometa 21 kwa wanaume akitumia muda wa saa 1:02:00 mna kujinyakulia zawadi ya Milioni tano.mshindi wa pili kuwa ni Mathayo Sombi kutoka JWTZ aliyetumia muda wa saa 1:02:10 na kuondoka na shilingi milioni mbili.
Kwa upande wa Wanawake waliokimbia kilometa 21 Hamida Nassoro kutoka Polisi aliongoza kwa muda wa saa 1:09:31 na kuzawadiwa Milioni tano huku nafasi ya Pili ikimwendea Neema Festo kutoka JWTZ aliyetumia dakika 1:12:47 na kuondoka na milioni 2 huku Failuna Adbi akishika nafasi ya tatu kwa muda wa 1:13:27 na kupewa milioni 1.
Mbio za Tanfoam marathon zimefanyika kwa msimu wa kwanza jijini Arusha huku zikitajwa kuwa ni mbio za kipekee zilizowavuta watu wengi zaidi
Mkurugenzi wa Tanfoam limited, Riaz Somji ambao ndio waandaji na wadhamini wakuu wa mbio hizi aliwashukuiru wote waliofika kushiriki bila kusahau wadau mbalimbali walioshirikiana kwa pamoja kufanikisha.
Mgeni rasmi katika mbio hizo kaimu mkurugenzi wa michezo kutoa Wizara ya Utamaduni sanaa na Michezo ,Boniface Tamba anawapongeza waandaaji wa Tanfoam marathon na kusema imekuwa mbio ambayo imeandaliwa vizuri na kusimamiwa vyema kwa kufuata taratibu
Aidha alisisitiza juu ya waandaaji wa mbio, wote kuhakikisha mbio zinasajiliwa Baraza la michezo la taifa na zifuate kanuni
Aliongeza kuwa wadau na tasisi mbalimbali waendelee kuunga mkono sekta hii ikiwa ni kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kufanikisha michezo
Naye mwenyekiti kamati ya maandalizi ya Tanfoam Marathon Glorious Temu alisema zaidi ya washiriki 1000 walishiriki mbio hizo kutoka makundi na taasisi mbalimbali.
Naye Mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo aliwapongeza Tanfoam kwa kuanzisha mbio hizo ambazo zilifanana ikiwa ni mara ya kwanza huku zikipambwa na zawadi nzuri kwa washindi.
“Mbio hizi ni katika kuunga mkono juhudi za Rais dkt. Samia Suluhu Hassan katika michezo ambaye anatujengea uwanja mkubwa wa mpira na kisasa jijini Arusha wa AFCON ambao umefikia hatua ya asilimia 11 mpaka sasa na katika uwanja huo umewekwa sehemu ya riadha hivyo suala la michezo linaleta ajira kwa ujumla na kuimarisha afya,”alisema Gambo.
Tanfom Marathon ilihusisha kilometa 21,10 na kilometa 5 ziliandaliwa na Tanfoam sports promoters ambapo washindi kumi kila kundi walipewa zawadi .Panga na Hamoida Nassoro wamefanikiwa kuibuka washindi katika Mbiop za riadha za TanFOAM Marathon zilizofanyika jijini Arusha.