Teknolojia ya Uhandisi jeni ina mchango mkubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

Mtaalamu wa Masuala ya Mabadiriko ya Tabia Nchi, kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,  Profesa Pius Yanda akizungumza na waandishi mara baada ya Kongamano na Maonyesho ya Tisa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yaliyoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Kongamano hilo la siku tatu limeanza jana Desemba 2,2024 na litamalizika  kesho Desemba 4, 2024 jijini Dar es Salaam

Mtaalamu wa Masuala ya Mabadiriko ya Tabia Nchi, kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,  Profesa Pius Yanda akizungumza katika Kongamano na Maonyesho ya Tisa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yaliyoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Kongamano hilo la siku tatu limeanza jana Desemba 2,2024 na litamalizika  kesho Desemba 4, 2024 jijini Dar es Salaam

Baadhi ya Wadau mbalimbali wakiwa katika Kongamano na Maonyesho ya Tisa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yaliyoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Kongamano hilo la siku tatu limeanza jana Desemba 2,2024 na litamalizika  kesho Desemba 4, 2024 jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu

Teknolojia ya Uhandisi jeni ina mchango mkubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, ikiwa ni pamoja na kupunguza kasi ya uzalishaji wa hewa ukaa.

Mtaalamu wa masuala ya mabadiliko ya tabia nchi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa   Pius Yanda amesema hayo katika Kongamano na maonyesho ya tisa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yaliyoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Yanda kutoka Taasisi ya usimamizi wa maliasili, mazingira na mabadiliko ya tabia nchi UDSM katika mada yake kuhusu mchango wa sayansi, teknolojia na ubunifu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi amesema

teknolojia hiyo imeanza kutumika  kwa kiasi kidogo kutokana na kutokuwa na teknolojia ya kutosha kuitumia.

“Uhandisi jeni unatumika kwenye maeneo mengi ikiwemo elimu, afya, kilimo na maeneo mengine hivyo kuna kila sababu ya kuhakikisha kuna ubunifu wa ziada kutumia teknolojia hii kwa kiasi kikubwa,” amesema.

Profesa Yanda amesema kwa kushirikiana na nchi zilizoendelea hususan katika utafiti, wanaweza kuwa na ubunifu bora zaidi wa matumizi ya uhandisi jeni kwa maendeleo ya Tanzania.

Amesema ubunifu wa ziada unahitajika ili kutumia rasilimali zilizopo kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

“Mabadiliko ya tabia nchi yanatuathiri zaidi Afrika na Tanzania hivyo, suala la kutumia bayoteknolojia kwa ajili ya kutengeneza uchumi, ni vema kuboresha ikolojia kwa kuboresha maisha ya watu, kipato na kuchangia uchumi wa nchi,” amesema.

Amesema Tanzania ikijikita katika teknolojia hiyo,  itanufaika na kupata maendeleo.

Kuhusu matumizi ya nishati safi, Profesa Yanda amesema Tanzania itakuwa mstari wa mbele katika matumizi ya nishati hiyo kwa kuhakikisha jamii inayoishi vijijini waweze kushiriki katika mkakati huo.

Amesema utashi wa kisiasa unaoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan unaibeba Tanzania kuwa mstari wa mbele katika kuongeza matumizi ya nishati safi na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Related Posts