TMA yatangaza mvua za siku tatu mfululizo mikoa minane, kuanza leo

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la mvua kubwa katika mikoa minane kuanzia leo Jumanne, Desemba 3, 2024.

Mvua hizo katika mikoa hiyo ya Dodoma, Singida, Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa, Songwe na Manyara.

Taarifa hiyo ya TMA iliyotolewa leo Desemba 3, 2024 imetahadharisha wakazi wa mikoa hiyo kuchukua tahadhari kutokana na wingi wa mvua hizo.

“Desemba 4, 2014 angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya nyanda za juu kusini magharibi mikoa ya Iringa, Njombe, Rukwa na Songwe.

“Kanda ya kati Dodoma na Singida na Mkoa wa Morogoro, athari zinazoweza kujitokeza ni makazi kuzungukwa na maji,” inasema TMA.

Vilevile, Desemba 5, 2024, TMA imeeleza uwepo wa mvua kubwa katika maeneo machache ya nyanda za juu kusini magharibi mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa na Songwe, kanda ya kati Dodoma na Singida.

Katika kipindi cha siku tatu TMA imeeleza athari zitakazoshuhudiwa kutokana na mvua hizo ni makazi ya watu kuzungukwa na maji ikitahadharisha watu wote katika mikoa husika kuchukua tahadhari.

Related Posts