Watatu washikiliwa mauaji ya mzee wa miaka 72 Kilimanjaro

Moshi. Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya Isaack Mallya (72), mkazi wa Kijiji cha Umbwe Onana, Kata ya Kibosho Magharibi, Wilaya ya Moshi.

Mwili wa Mallya, ulikutwa jana Desemba 2, 2024 umetelekezwa nje ya nyumba yake ukiwa na majeraha sehemu mbalimbali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao leo Jumanne, Desemba 3, 2024.

Amesema chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika lakini wanaendelea kuwahoji watuhumiwa hao ili kubaini chanzo.

“Tunawashikilia watuhumiwa watatu kuhusiana na mauaji ya mzee wetu, tunaendelea kuwahoji ili kubaini chanzo cha mauaji hayo,”amesema Kamanda Maigwa.

Kaka wa marehemu, Patrick Boisafi ambaye ni  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, jana alieleza  kusikitishwa na ukatili huo na kusema wameliachia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wake kubaini waliohusika ili sheria ichukue mkondo wake.

Endelea kufuatilia Mwananchi.

Related Posts