KIPA wa Simba, Aishi Manura ameshindwa kuendelea na safari baada ya kupata shida ya kiafya muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kwenda nchini Algeria.
Kikosi hicho chini ya kocha Davis Fadlu kinakwenda Algeria kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika wa hatua ya makundi itakaocheza dhidi ya CS Constantine, Jumapili, wiki hii.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Simba, kipa huyo alipata hitilafu hiyo muda mfupi kabla ya ndege kupaa alfajiri ya leo.
Simba imeondoka alfajiri na ikiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, ndipo kipa huyo alipopata shida ya kiafya.
Timu hiyo imeondoka na wachezaji 21 ambao ni makipa wawili Moussa Camara na Ally Salim; mabeki Che malone, Karaboue Chamou, Abdurazack Hamza, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Valentine Nouma na Kelvin Kijili.
Viungo ni Mzamiru Yassin, Debora Fernandez, Fabrice Ngoma, Ladack Chasambi, Augustine Okejepha, Omary Omary, Edwin Balua, Kibu Denis, Jean Charle Ahoua na Awesu Awesu.
Eneo la ushambuliaji imeondoka na wachezaji wawili ambao ni Leonel Ateba na Steven Mukwala.