RAIS MSTAAFU, DKT. KIKWETE AKUTANA NA MWENYEKITI WA BODI YA GPE

RAIS Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Elimu la Kimataifa (GPE) ameongoza vikao vya bodi ya taasisi hiyo leo Jijini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Vikao hivyo vimefunguliwa na Mhe. Reem Al Hashimy, Waziri wa Umoja wa Falme za Kiarabu anayeshughulikia Ushirikiano wa Kimataifa. Umoja wa Falme za Kiarabu umekuwa ni mdau muhimu wa GPE kwa miaka kadhaa sasa.

Katika vikao hivyo, pamoja na wajumbe mbalimbali wakiwakilisha nchi, mashirika ya kimataifa, vyama vya kiraia kutoka kote duniani, n.k, vilihudhuriwa pia na Mhe. Prof. Nasser Al Aqeeli, Naibu Waziri wa Elimu wa Ufalme wa Saudi Arabia akiwasilisha nia ya Ufalme wa Saudia kuendelea kushirikiana na GPE katika kutatua changamoto za elimu msingi (chekechea, msingi na sekondari) katika nchi zinazoendelea.

Kulia kwa Mheshimiwa Rais Mstaafu ni Mheshimiwa Prof. Nasser Al Aqeeli, Naibu Waziri wa Elimu wa Ufalme wa Saudi Arabia. Kushoto kwa Mheshimiwa ni Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya GPE Christine Hogan na Mheshimiwa Waziri Reem Al Hashimy, Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Umoja wa Falme za Kiarabu.

Related Posts