Samia afuta sherehe za Uhuru, fedha kusaidia huduma za kijamii

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kufuta sherehe za miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara na badala yake fedha hizo zitumike kusaidia huduma za kijamii.

Amesema fedha zilizotengwa katika kila taasisi kwa ajili ya maadhimisho hayo zielekezwe katika kutoa huduma za kijamii, huku akieleleza kila mkoa uhakikishe wilaya zake zinafanya shughuli za kijamii, ikiwemo upandaji miti, usafi wa mazingira kwenye maeneo ya kijamii kama masoko, hospitali, kumbi za wazee na wenye mahitaji maalumu.

Hayo yameelezwa leo Jumatano, Desemba 4, 2024 na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa katika kikao kazi cha mawaziri kilichofanyika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma. “Sherehe za mwaka huu hazitakuwa na gwaride na shughuli nyingine za kitaifa”.

Amesema Serikali inatoa wito kwa wananchi kushiriki katika shughuli hizo, ili kujivunia sifa za kipekee ambazo zimetokana na Uhuru wetu.

“Ninatoa rai kwa wakuu wote wa mikoa ya Tanzania Bara, kuzingatia na kufuata ipasavyo maelekezo mahsusi yaliyotolewa na Serikali ili kuhakikisha maadhimisho haya yanafanyika kwa ufanisi kwa lengo la kuuenzi Uhuru wetu.”

Endelea kufuatilia Mwananchi.

Related Posts