Taasisi ya GSM Foundation yaendelea kuchangia jitihada za Serikali katika uhifadhi wa taka kwa Shule za Msingi

Katika jitihada zake za kuimarisha utunzaji wa mazingira nakukuza elimu ya uhifadhi wa taka kwa wanafunzi wa shule za msingi, Taasisi ya GSM Foundation imetoa msaada wa vifaavya kuhifadhia taka kwa Shule ya Msingi Jangwani Beach, Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na usimikaji wa mapipa 12 yakuhifadhia taka kwa matumizi ya nje ya madarasa, vipipa taka25 vya ndani ya madarasa, toroli moja la usafirishaji wa takana kubandika mabango 50 yenye jumbe za kimazingirakwenye mazingira ya shule.

Mpango huu ni sehemu ya dhamira ya GSM Foundation yakusaidia utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kimkakati waHifadhi ya Mazingira wa mwaka 2022-2032, (NATIONAL ENVIRONMENTAL MASTER PLAN FOR STRATEGIC INTERVENTIONS 2022–2032) unaolenga kuboreshausimamizi wa taka na mazingira nchini.

Akizungumza wakati wa makabidhiano, Mkuu wa taasisi yaGSM Foundation, Bi. Faith Gugu alisema…
”Mkakati wetu ni zaidi ya utoaji wa vifaa vya kuhifadhi taka. Tunakusudia kukuza uwajibikaji wa kimazingira kwa watotowetu kwa kuwapa elimu ya mbinu bora za usimamizi wa taka. Lengo ni kuwawezesha wanafunzi hawa kuwa mabalozi wamazingira safi katika familia na jamii zao, hivyo kuletamabadiliko ya kudumu na kupunguza athari zitokanazo namabadiliko ya tabianchi.”

Mbali na msaada huu kwa Shule ya Msingi Jangwani Beach, GSM Foundation tayari imetoa vifaa vingine na kuhamasishaelimu ya mazingira kwa shule za msingi tatu katika Wilaya yaKinondoni. Jitihada izo zilihusisha utoaji na usimikijai wamapipa taka 55, vidumutaka 65 vya ndani ya madarasa, namatoroli matano, ambavyo vimewanufaisha wanafunziwapatao zaidi ya 5,000 na walimu zaidi ya 200.

Pia, jumla ya mabango 200 yenye ujumbe wa elimu yamazingira yamewekwa katika maeneo tofauti mashuleni, hukuShule ya Msingi Jangwani Beach ikipokea mabango 50. Mabango haya yanasaidia kuhamasisha uwajibikaji wamazingira miongoni mwa wanafunzi na jamii zinazozungukashule hizo.

Aidha, mpango huu unalenga pia kuleta manufaa ya kiuchumikwa jamii kupitia uhifadhi sahihi wa taka, ambapo taka zinazoweza kuchakatwa zitakuwa chanzo cha kipato kwafamilia zilizo karibu na shule.

“Tunaamini kuwa kila hatua ni muhimu,” alisema Bwana. Rajabu Kondo, Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni yaGSM. “Kwa kushirikiana, tunaweza kuleta mabadiliko yakudumu katika usimamizi wa mazingira na kujenga jamiiendelevu.”

GSM Foundation imepanga kuendeleza juhudi hizi kwa kutoa msaada wa vifaa vya kuhifadhi taka kwa shule moja kilamwezi hadi Juni 2025.

 

Related Posts