Dar es Salaam. Mikoa inayopata huduma ya umeme katika gridi ya Taifa imekosa umeme kutokana na hitilafu iliyojitozea.
Hayo yamebainishwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kutokana na hitilafu iliyojitokeza katika mfumo wa gridi ya Taifa leo asubuhi ya Desemba 4, 2024.
“Tunautaarifu umma kuhusu hitilafu iliyojitokeza katika mfumo wa Gridi ya Taifa leo Disemba 4, 2024 majira ya saa 04:03 asubuhi, hitilafu hiyo imepelekea mikoa inayopata umeme katika gridi ya Taifa kukosa umeme,” imeeleza taarifa hiyo.
Tanesco imesema timu ya wataalamu inaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha hitilafu hiyo.
Aidha, imeongeza kuwa umeme kwa sasa umeanza kurejea kwa awamu katika mikoa iliyokuwa inakosa umeme na jitihada zinaendelea kuhakikisha mikoa yote inapata umeme.
“Shirika linawaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza, na litaendelea kutoa taarifa za hali ya urejeshaji wa huduma ya umeme kwa kadri hali inavyoimarika,” imehitimisha taarifa hiyo.
Endelea kufuatilia Mwananchi na mitandao yake kwa habari zaidi.