TASAF YAPONGEZA JITIHADA ZINAZOFANYWA NA WALENGWA WENYE ULEMAVU KUPAMBANA NA UMASIKINI

 

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI
wa Miradi wa TASAF John Steven amewapongeza watu wenye ulemavu kutoka
katika Kaya za Walengwa kwa jitihada wanazoonesha katika kupambana na
umaskini.

Hayo ameyasema Desemba 3,2024 alipotembelea banda la
TASAF la Walengwa wenye Ulemavu katika kuadhimisha Siku ya Watu Wenye
Ulemavu duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

“TASAF
inafarijika sana kuona mko vizuri katika kupambana na Umaskini na hakika
mnautendea haki msaada mnaopewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –
TASAF”, alisema Bw. Steven.

Kwa upande wake Bi. Amina Ally, mkazi
wa Mlandizi mwenye Ulemavu wa Miguu, ameishukuru sana TASAF na Serikali
kwa kuwashika mkono watu wenye Ulemavu maana ameweza kuanzisha biashara
ya kùuza batiki, viungo vya chakula, shanga na karanga.

“Nikikumbuka TASAF ilikonitoa, namshukuru Mungu maana sijui ningekuwa wapi nikifanya nikifanya nini?”

TASAF
imeshiriki kwenye maadhimisho hayo kwa mara ya kwanza tangu kuasisiwa
kwake baada ya kuongeza afua ya watu wenye Ulemavu katika Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini.

Katika maadhimisho hayo, Walengwa wameweza
kuonesha mtaalam wao wa kusuka, kufuma, kuchakata viungo vya chakula na
utengenezaji wa sabuni za maji kwa mtumizi mbalimbali pamoja na batiki.

Aidha
viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Vijana
Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe Ridhiwani Kikwete na Naibu Katibu Mkuu
ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana Ajira na Watu wenye Ulemavu Bi Zuhura
Yunus ni miongoni mwa waliotembelea Banda la walengwa hao wa TASAF.

Naibu Waziri Mkuu Mhe Dkt Dotto Biteko akikagua Mabanda katika kuadhimisha siku ya watu wenye Ulemavu duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF akiongea na mlengwa katika banda la TASAF katika kuadhimisha siku ya watu wenye Ulemavu duniani.

Naibu Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana Ajira na Watu wenye Ulemavu Bi Zuhura Yunus alipotembelea banda la TASAF katika kuadhimisha siku ya watu wenye Ulemavu duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa diamond jubilee Jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe Ridhiwani Kikwete alipotembelea banda la TASAF katika kuadhimisha siku ya watu wenye Ulemavu duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa diamond jubilee Jijini Dar es Salaam leo.

Related Posts