Mratibu wa masuala ya kiutu wa Umoja wa Mataifa Tom Fletcher amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwamba ulimwengu unateketea, na kukiri kwamba anausubiria mwaka wa 2025 kwa hofu kubwa. Kwenye uzinduzi wa Tathmini ya Kimataifa ya Hali ya kiutu. Fletcher amesema mizozo mikubwa huko Gaza, Sudan na Ukraine pamoja na mabadiliko ya tabianchi vinachochea zaidi hali hiyo.