Wadau wa Run for Binti Watoa Elimu Mkoani Mtwara

LSF kwa kushirikiana na Smile for Community, Stanbic Bank, Girl Guide Tanzania, na Marie Stopes wameendesha kampeni ya kutoa elimu kwa wanafunzi, wazazi, na jamii ya Mnyawi, katika wilaya ya Nanyamba, mkoani Mtwara. mafunzo hayo yamefanyika siku moja kabla ya kukabidhi rasmi ujenzi wa vyoo, taulo za kike za kujisitiri, na kupanda miti kwa ajili ya utunzaji wa mazingira.

Wananchi walipata fursa ya kujifunza kuhusu masuala mbalimbali muhimu, yakiwemo:

Ukatili wa Kijinsia: Uelewa juu ya namna ya kuutambua, kuzuia, na kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Elimu ya Fedha: Mafunzo ya usimamizi wa fedha kwa wanafunzi na wazazi ili kuboresha hali ya maisha.

Hedhi Salama: Uhamasishaji juu ya matumizi sahihi ya taulo za kike na umuhimu wa usafi wa mwili wakati wa hedhi.

Utunzaji wa Mazingira na Nishati Safi ya Kupikia: Uhamasishaji kuhusu kupanda miti, kuhifadhi mazingira, na kutumia nishati salama kama mbadala wa kuni na mkaa.

Elimu hii inalenga kuimarisha ustawi wa jamii, kupunguza changamoto za kiafya, na kuboresha mazingira kwa kizazi cha sasa na kijacho.





Related Posts