Mbibo ameyasema hayo Desemba 04, 2024 Jijini Tanga wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Wanajiosayansi kwa niaba ya Waziri wa Madini.
Ndugu Mbibo amesema kuwa Wizara ya Madini inatambua nafasi na mchango wa wanajiosayansi katika Vision 2030 hivyo itaendelea kuwatumia kikamilifu ili kuwezesha utekelezaji wa dhana hii.
“Katika kufanikisha Vision 2030, wanajiosayansi wameendelea kutumia utaalamu wao katika kufanya utafiti wa kina wa kijiofizikia kwa kutumia teknolojia za kisasa kwa lengo la kutambua tabia za miamba. Utambuzi huu utawezesha kufanyika kwa tafiti nyingine za jiosayansi zenye kuwezesha kubaini aina mbalimbali za madini yapatikanayo nchini ” alieleza Mbibo.
Mbibo, kwa niaba ya Wizara ya Madini, aliwashukuru wanajiosayansi kwa utayari wao wa kubeba maono ya Vision 2030 na kutoa msaada wa kitaalamu katika kufikia utekelezaji wake.
Kupitia dhana ya Vision 2030, Wizara ya Madini inalenga kufanya tafiti za kina kwa angalau asilimia 50 kufikia asilimia 2030, ukilinganisha na sasa ambako ni asilimia 16 pekee ndiyo imefanyiwa utafiti wa kina kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Wanajiosayansi Tanzania
wakifuatilia hotuba ya ufunguzi. Mkutano huo unaoleta pamoja
wanajiosayansi kutoka ndani na nje ya nchi umefunguliwa rasmi Desemba
04, 2024 Jijini Tanga na utahitimishwa Desemba 06, 2024.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Ndg. Msafiri Mbibo akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wanajiosayansi Tanzania 2024. Mkutano huo wa siku tatu umefunguliwa leo Desemba 04, 2024 na utahitimishwa Desemba 06, 2024.