WANANCHI WILAYANI ARUMERU WACHANGAMKIA MAJIKO YA GESI YA RUZUKU

-Waipongeza Serikali kwa kuja na mpango huo

Wananchi wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha wameipongeza Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa mradi wa usambazaji na uuzwaji wa majiko ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50%

Wametoa pongezi hizo kwa nyakati tofauti katika Kata ya Maji ya Chai Wilayani Arumeru Desemba 4,2024 wakati wa zoezi la uuzaji wa majiko hayo wilayani hapo.

“Tunaipongeza Serikali kwa kuja na mpango huu; ambao unakwenda kutupunguzia madhara yanayosababishwa na matumizi ya kuni kupikia,” amesema Joan Palangyo mkazi wa Kata ya Maji ya Chai.

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatekeleza mradi wa kusambaza majiko ya gesi (LPG) ya kilo sita kote nchini ikiwa ni hatua ya kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ambao umelenga ifikapo mwaka 2034 asilimia 80 ya watanzania wawe wameachana na matumizi ya nishati isiyo safi na salama.




Related Posts