Wawili mbaroni tuhuma za kumuua mwenyekiti wa UVCCM Makongorosi

Mbeya. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) ,Tawi la Machinjioni, Kata ya  Bwawani  Michael Kalinga (36) mkazi wa Makongorosi wilayani Chunya .

Kaimu Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Mbeya,Wilbert Siwa akizungumza na vyombo vya habari  leo Jumatano, Desemba 4, 2024  amesema  tukio hilo lilitokea usiku wa Jumatatu,  Desemba  2, 2024 saa 5.30 usiku eneo la Mianzini  Kata ya Mkola.

Amesema mwenyekiti huyo ameuawa kwa kupigwa na kitu butu sehemu ya utosini kwake kisha mwili wake kutelekezwa umbali wa mita 250 kutoka barabara ya Makongorosi kuelekea Lupa tingatinga.

“Baada ya kutokea mauaji hayo Jeshi la Polisi lilifanya msako ambapo  jana Desemba 3, 2024 huko Mji wa  Mlowo, Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe tulifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwa na pikipiki iliyokuwa ikitukiwa na marehemu yenye namba za usajili MC 464 ELL,”amesema Siwa.

Siwa amesema watuhumiwa hao (majina yamehifadhiwa) baada ya kuhojiwa na wamekiri kuhusika na mauaji ya mwenyekiti huyo  na kisha  kupora pikipiki aliyokuwa akitumia.

Taarifa kamili itakujia hivi punde

Related Posts