Waziri Ulega Awafunda TVA Kusimamia Taaluma ili Kuondokana na Makanjanja.

 

Na Jane Edward, Arusha 

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega amewataka madaktari wa wanyama nchini kutumia taaluma yao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuepukana na makanjanja ambao wamekuwa wakiuza dawa feki na kuleta athari kwenye Mifugo. 

Akizungumza  wakati wa ufunguzi wa kongamano la 42 la Wataalamu wa Chama cha Madaktari wa Wanyama (TVA)Mkoani Arusha kwa niaba ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan .

Ulega amesema kuwa,amesikia ombi lililotolewa na viongozi wao kuhusu serikali kuajiri madaktari wasaidizi katika maeneo mbalimbali kwani waliopo hawatoshi ili waweze kutoa huduma hiyo hadi maeneo ya vijijini .

“Ombi lenu nimelisikia kuhusu kuajiri madaktari wengi ambao watasambaa katika maeneo mbalimbali ya nchi ili huduma iweze kutolewa kwa urahisi kwa wananchi,na ombi hilo nitalifikisha kwa Rais Samia kama mlivyoniomba.”amesema .

Aidha Ulega amesema kuwa serikali imetenga shilingi Bilioni 460 kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwa ajili ya kuboresha sekta ya mifugo pamoja na kuongeza thamani ya biashara ya mifugo nje ya nchi ambapo kati ya hizo bilioni 28.1 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa chanjo ya mifugo nchini.

Ulega amesema kuwa katika ukuaji wa uchumi pamoja na Afya bora kwenye jamii kwa miaka ya hivi karibuni imebainishwa kuwa na ongezeko kubwa la magonjwa yatokayo kwa wanyama na kuja kwa binadamu.

“Kulingana na umuhimu huo Serikali imeanza kuchukua hatua za haraka kukabiliana na changamoto hiyo ili kutokomeza kabisa changamoto hiyo na kuendelea kukuza uchumi wa nchi yetu.”amesema Ulega .

Mwenyekiti wa chama hicho, Prof Esron Karimuribo amesema kuwa, amemshukuru Waziri kwa kuja kufungua mkutano huo kwani ameonyesha mapenzi mema na chama hicho .

Prof.Esron amesema kuwa ,malengo ya kuzungumza namna ya kutokomeza magonjwa ya Mifugo ili kuongeza tija ya uzalishaji huku malengo mengine ikiwa ni pamoja na kuimarisha biashara ya Mifugo na mazao yake ndani na nje ya nchi .

 Prof . Karimuribo amewataka kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanatokomeza magonjwa ya mifugo hapa nchini ili mifugo iweze kuuzwa nje ya nchi na serikali kuongeza pato la nchi.

Baadhi ya wadau wa sekta ya mifugo wakizugumzia umuhimu wa kongamano hilo ,Salim Msellem kutoka Kampuni ya Farmers Centre /Farmbase amesema kuwa,amemshukuru Rais Samia kwa kutengeneza mazingira mazuri ya wataalamu wa Mifugo ambao watahakikisha sekta hiyo inakuwa kwa kasi na kuheshimika.

Related Posts