Droo ya Klabu Bingwa Dunia kufanyika leo

Droo ya mashindano mapya ya kombe la Dunia kwa ngazi ya Klabu itafanyika leo Marekani ambapo jumla ya timu 32 zitagawanywa kwenye makundi nane ya timu nne.

Awali, mashindano haya yalikuwa yanafanyika kila mwaka na kushirikisha timu saba bora kutoka mabara sita (AFC, CAF, Concacaf, Conmebol, OFC, na UEFA) lakini sasa yatakuwa na timu 32 na kufanyika kila baada ya miaka minne.

Timu zilizofuzu kucheza mashindano haya ni zile ambazo zilifanya vizuri kwenye mashindano ya Klabu Bingwa misimu minne iliyopita ambayo hufanyika kila Bara ambapo Bara la Ulaya (UEFA) limeongoza kwa kutoa timu 12, Afrika (CAF), Asia (AFC)  na Amerika ya Kaskazini (Concacaf), zitatoa timu nne kila mmoja wakati Amerika ya Kusini (Conmebol) yenyewe itatoa timu sita huku Bara la Oceania (OFC) litatoa timu moja.

Kila timu itacheza mara moja na timu nyingine katika kundi lake, timu mbili zitakazo maliza nafasi za juu kutoka kila kundi zitafuzu hatua ya mtoano ambapo hakutakuwa na mchezo wa kuwania nafasi ya tatu na mchezo wa fainali utafanyika tarehe 13 Julai 2025.

Droo ya makundi ya Klabu Bingwa Dunia imepangwa kufanyika leo Desemba 5, 2024 saa 3:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Pot 1: Manchester City, Real Madrid, Bayern Munich, PSG, Flamengo, Palmeiras, River Plate, Fluminense

Pot 2: Chelsea, Borussia Dortmund, Inter Milan, Porto, Atletico Madrid, Benfica, Juventus, Salzburg

Pot 3: Al Hilal, Ulsan, Al Ahly, Wydad Casablanca, Monterrey, Club Leon, Boca Juniors, Botafogo

Pot 4: Urawa Red Diamonds, Al Ain, Esperance de Tunis, Mamelodi Sundowns, Pachuca, Seattle Sounders, Auckland City, Inter Miami

Timu zinazowakilisha Afrika ni:

Wydad Casablanca (Morocco)

Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)

Espérance de Tunis (Tunisia)

Al Ahly na Wydad Casablanca zimepangwa katika poti ya tatu, zikiwa na rekodi nzuri kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika wakati Mamelodi Sundowns na Espérance de Tunis ziko katika poti ya nne.

FIFA imetangaza kuwa hakuna timu mbili kutoka shirikisho moja zitakazopangwa kundi moja, isipokuwa vilabu vya Ulaya ambavyo vimepata nafasi 12 katika mashindano haya.

Mashindano haya yamepangwa kuanza kutimua vumbi Juni 15, hadi Julai 13, 2025. Viwanja 12 vitatumika ambapo mchezo wa ufunguzi utafanyika kwenye uwanja wa Hard Rock uliopo Miami, Florida na mchezo wa fainali uatapigwa kwenye uwanja wa MetLife uliopo New Jersey, Marekani.

Viwanja vingine vitakavyotumika

Atlanta, Mercedes-Benz, Charlotte TQL, Cincinnati, Bank of America, Los Angeles, Rose Bowl, Miami Hard Rock, Nashville GEODIS Park, New Jersey, MetLife, Orlando, Camping World, Orlando, Inter&Co, Philadelphia, Lincoln Financial Field, Seattle, Lumen Field, Washington DC, Audi Field

Related Posts