Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital
Kampuni ya Mawasiliano ya Halotel imezindua Kampeni mpya inayofahamika kama ‘Data na Kiwashe’ ikiwa ni moja ya zawadi kuelekea msimu wa sikukuu ikijikita katika kumpa mteja nafasi ya kujishindia simu mbalimbali ikiwamo Samsung A15 na A35 kupitia mfumo wa ‘Lucky Droo’ yaani Droo ya Bahati hasa kwa wateja wapya wanaojiunga vifurushi vya intaneti na combo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 5,2024 jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Halotel, Roxana Kadio, amesema mafanikio ya kampuni hiyo hayawezi kutenganishwa na wateja wanaotumia mtandao huo, hivyo ina jukumu la kuboresha huduma za kila siku na wateja waweze kupata zawadi mbalimbali kama shukrani.
Amesema zawadi hizi zitakuwa zinatolewa kwa wiki mara moja ambapo ili kushiriki wateja watatakiwa kujiunga vifurushi vya siku, wiki na mwezi pamoja na kifurushi cha combo.
“Lengo la kampeni hii ni kutoa huduma bora kwa wateja wetu na shukrani kwa wateja kwa kuwa wamekuwa nasi kwa kutuunga mkono na kuchagua mtandao wetu wa Halotel, ” amesema Kadio.
Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Biashara wa Halotel, Salum abdalah, amesema kuwa wateja wanahimizwa kutumia fursa hiyo kwani wataweza kujipatia zawadi mbalimbali kupitia kampeni ya Data na Kiwashe ambapo wateja wapya watweza kupata zawadi katika kampeni hiyo iliyoanza rasmi leo hadi Januari 2025.
“Wateja wetu watakaponunua vifurushi vya halotel moja kwa moja wataingia katika fursa ya kujishindia zawadi zetu na simu aina ya Samsung kuanzia sasa hivyo watumie fursa hii vema,”amesema Salum.