MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AANDAA KIKAO KAZI KUJADILI MASUALA YA KIUTENDAJI KATIKA UTOAJI HUDUMA ZA SHERIA SERIKALINI

Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Mwanasheria Mkuu wa Serikali aandaa kikao kazi kujadili masuala ya kiutendaji katika utoaji huduma za Sheria Serikalini.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari ameyabainisha hayo jijini Dodoma katika mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia kikao hicho kitakachofanyika kesho katika ukumbi wa jiji-Mtumba Mkoani humo.

“kupitia kikao hicho pamoja na mambo mengine tutakumbushana umuhimu wa kuzingatia sheria, taratibu, mipango ya maendele, dira na miongozo mbalimbali ya a Serikali tunayopaswa kuzingatia wakati wa uwekezaji wa majukumu yetu ya kila siku”

Katika kikao hicho mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.

Mwanasheria Mkuu huyo wa Serikali amesema pamoja na mambo mengine katika kikao hicho watajikita zaidi kujadili -:

– Taarifa za utekelezaji wa kazi za Mawakili wa Serikali

– Ushirikiano na umoja baina ya Mawakili na Serikali

– Changamoto za Mawakili wa Serikali

– Maadili Kwa Mawakili wa Serikali

– Utekelezaji wa miongozo inayotolewa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

– Umuhim wa ushirikishwaji wa Mawakili wa Serikali katika mambo yanayohitaji ushauri wa kisheria

Hata hivyo Mwanasheria Mkuu wa Serikali mesema anatarajia kikao kazi hicho kitazaa matunda mema kwani kitatoa huduma bora za kisheria Serikali.

“Mawakili wa Serikali ni Jeshi ambalo linalinda uchumi wa nchi kwa kutumia kalamu, naamini maelekezo ya Serikali nitakayotoa kupitia kikao hicho muhimu yatatekelezwa ili kuleta maendeleo Kwa wananchi”

Related Posts