Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Mchemba akizungumza leo Desemba 05, 2024 jijini Dar es Salaam na wakati wa mdahalo wa mstakabali wa ulinzi wa jamii katika kupunguza umasikini nchini, mdahalo huo umefanyika katika Ukumbi Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT). Pia Serikali imependekeza kuendelea kwa Miradi wenye Tija kwa Jamii.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Jakaya Kikwete akizungumza leo Desemba 05, 2024 jijini Dar es Salaam na wakati wa mdahalo wa mstakabali wa ulinzi wa jamii katika kupunguza umasikini nchini, mdahalo huo umefanyika katika Ukumbi Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT). Pia Serikali imependekeza kuendelea kwa Miradi wenye Tija kwa Jamii
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania, Nadhan Belete akizungumza leo Desemba 05, 2024 jijini Dar es Salaam na wakati wa mdahalo wa mstakabali wa ulinzi wa jamii katika kupunguza umasikini nchini, mdahalo huo umefanyika katika Ukumbi Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT). Pia Serikali imependekeza kuendelea kwa Miradi wenye Tija kwa Jamii
Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
SERIKALI kuendeleza na kudumisha kasi ya kusaidia kaya maskini na zilizo katika mazingira magumu ili kuboresha maisha yao na kupunguza umaskini kwa kuzingatia Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025 na Dira ya Zanzibar 2050.
Hayo yamesemwa leo Desemba 05, 2024 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Mchemba wakati wa mdahalo wa mstakabali wa ulinzi wa jamii katika kupunguza umasikini nchini, mdahalo huo umefanyika katika Ukumbi Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT). Pia Serikali imependekeza kuendelea kwa Miradi wenye Tija kwa Jamii.
Dkt. Mwigulu amesema juhudi ya serikali ni kupanua wigo wa ulinzi wa jamii, huku ikiboresha ufanisi wa programu zilizopo, na kuunganisha masuluhisho ya kidijitali ambayo ni muhimu katika kufikia idadi ya watu inayolengwa na muhimu kwa ajili ya kuunda mfumo wa ulinzi wa kijamii unaolingana zaidi na ustahimilivu.
“Serikali ya Tanzania chini ya usimamizi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akisimama mbele, kama marafiki na washirika wa maendeleo, na kutoa wito kwa uungaji mkono wa dhamira thabiti ya rasilimali ya PSSN III katika kuboresha na kuendeleza maisha ya watu maskini na watu wanaoishi katika mazingira magumu.” Amesema
Pia Dkt. Mwigulu amesisitiza dhamira ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwa na programu ambazo zitasimamia usalama wa jamii ambayo inakabiliana na umaskini na program ambazo zimeundwa kwa maono yaliyobuniwa yenye uwiano, endelevu, shirikishi na kwa Maendeleo ya watu.
Mifuko iliyoanzishwa ni Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) mwaka 2000 ambao unatekeleza programu za nchi nzima za usalama wa jamii kupitia Miradi ya Mtandao yenye Tija kwa Jamii na kuanzishwa kwa Sera ya Kitaifa ya Hifadhi ya Jamii ya 2023.
Pamoja na mambo mengine, imewezesha Tanzania kupunguza umaskini uliokithiri kutoka asilimia 28.2 mwaka 2011 hadi 26.4% mwaka 2018.
Pia serikali inategemea idadi ya watu masikini itabadilika kwa kiasi kikubwa, kwani serikali imeanza maandalizi ya Utafiti wa Kaya masikini katika Bajeti yake ya 2024-25.
Akifunga Mdahalo huo Waziri wa chi, ofisi ya Waziri Mkuu, Menejiment Utumishi wa Umma, Ridhiwani Kikwete amesema kuwa mdahalo huo wa leo ulete maendeleo katika kupunguza umasikini katika kaya hapa nchini.
Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF, Shedrack Mziray amesema kuwa mpango kunusuru kaya masikini unahudumia kaya milioni moja na laki tatu,(1,300,000) lakini tathmini imefanyika kuona kaya ambazo zimeboreka kimaisha ni laki nne (400,000) ambazo watahitimisha kuzihudumia katika mpango huo wa kunusuru kaya masikini.
“Mpango umefanikiwa, tuliwapa taarifa kaya takribani laki nne kuwaondoa kwenye mpango huo kutokana na kuona kuwa sio masikini sana, kwa hiyo tunapokwenye kwenye mwaka mmoja wa kukamilisha tumebakiwa na kaya takribani laki tisa na nusu ambazo tutaendelea nazo.” Amesema
Licha ya hayo ameeleza kuwa changamoto ambayo wanakumbana nayo ni kaya masikini kutojiondoa katika mpango huo wa kunusuru kaya masikini licha ya kwamba kwa sasa TASAF kwa kushirikiana na Serikali imetengeneza sheria ya kuwaondoa katika mpango huo kaya nufaka kwa miaka mitatu mitatu ingawa kuna baadhi ya kaya kama za wazee na watu wenye ulemavu kuendelea kubakia kutokana na hali zao.
“Nia ya Serikali ni kuwaondoa kwenye umasikini lakini sio kaya kukaa milele kwenye mpango. Na mpango wa sasa tukiingiza kaya itakaa takribani miaka mitatu tu.” Amesema
Akizungumzia kuhusu uapande wa Zanzibar Saada Mkuya amesema pia wao ni wanufaika wa mpango huo wa Kunusuru kaya Masikini kwa kujenga skuli na kuwapatia shilingi elfu 14 kwa kila mwenzi kwa kila kaya pamoja na kuwapeleka watoto shule na kuwapatia huduma za afya bila masharti huku wengine wakipewa mitaji ya kufuga kuku.
Pia amesema TASAF imewapatia msada wa kujenga matuta makubwa ili maji yasiingie kwenye mashamba ya mazao yao. “Na hii imewasaidia sana kuweza kupata mazao.”
Wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwa kwenye mdahalo wa kujadili namna ya upatikanaji wa fedha kwaajili ya kunusuru kaya Masikini nchini.