Wasomi wahamasisha kufanya tafiti kukabili athari mabadiliko ya tabianchi

Mbeya. Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (Must),  Kampasi ya Mbeya kimeanza mikakati ya kutenga maeneo kwa ajili ya kufanya  tafiti za kisayansi na  bunifu kwa kuhamasisha wahadhiri  na vijana vyuoni  kushiriki katika tafiti hizo.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Must ,Profesa Aloyce Mvuma amesema hayo Jumatano, Desemba 4, 2024 kwenye mdahalo wa wazi ulioshirikisha wanafunzi na mtaalamu mbobezi wa masuala ya  mabadiliko ya tabianchi, kilimo na lishe kutoka Chuo  Kikuu cha Sokoine (Sua).

“Tunahamasisha wahadhiri na vijana kutenga maeneo ya kufanya bunifu za tafiti za  kisayansi katika  masuala ya kilimo na lishe ili kupata njia bora ya kuleta tija ya uzalishaji  mazao yaliyo ya lishe bora,” amesema Profesa Mvuma.

Profesa Mvuma amesema programu hiyo imekuja baada chuo hicho kufungua  ndaki ya tafiti ya kilimo, sayansi na teknolojia lengo ni kutoa mafunzo ya kilimo na bunifu ili kuleta chachu katika sekta hiyo hususani kwa wakulima.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), Profesa Benard Chove amesema mabadiliko ya tabianchi yanatokana na changamoto ya ukataji wa miti unaosababisha uzalishaji wa hewa ya ukaa na kusababisha chakula kuzalishwa kwa wingi na kukosa ubora.

Amesema umefika wakati sasa maofisa kilimo wataalamu wa kilimo kutumia tafiti zinazofanywa nchini ili kuleta muunganiko wa kuwasadia wakulima.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Must, Profesa Godliving Mtui amesema kabla hawajafanya tafiti huandika wazo kwa kuangalia maeneo ya kimkakati.

Amesema mabadiliko ya tabianchi yameleta athari kubwa ya ubora wa chakula kukosa radha kutokanana mbegu zinazo pandwa kuathiriwa.

Ametaja sababu ni vipindi virefu vya joto na mvua nyingi uathiri ubora wa vyakula hivyo umefika wakati tafiti zinazofanywa kupewa kipaumbele ili kusaidia kuokoa sekta ya kilimo.

Mkulima  wa Kata ya  Songwe Wilaya ya Mbeya Vijijini, Witness Kamwela amesema asilimia kubwa ukosefu wa elimu  ya kukabiliana na athari za  mabadiliko ya tabia nchi imekuwa mwiba kwao katika uzalishaji na kuomba Serikali kutumia tafiti zinazofanywa ili kuwanusuru.

Related Posts