Zanzibarr kuwa kituo kikubwa cha Utalii wa kisasa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana mgeni wake Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Marianne Young, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika leo 5-12-2024, katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar. (Picha na Ikulu)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Mhe. Marianne Young, mazungumzo hayo yaliyofanyika leo 5-12-2024, katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar. (Picha na Ikulu)

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar, imesema inakusudia kuifanya Zanzibar kuwa kituo kikubwa cha Utalii wa kisasa usio na misimu kwa kuwavutia wawekezaji na wageni wengi.

Imesema Zanzibar bado inawakaribisha wawekezaji zaidi kwani ina maeneo mengi ambayo hayajafikiwa kwa kwa fursa nyingi za uwekezaji.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameyasea hayo Ikulu – Zanzibar alipozungumza na Balozi mpya wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Marianne Young alikuja kujitambulisha.

Dk. Mwinyi amesema bado ina Zanzibar ina uhitaji mkubwa wa uwekezaji kwenye sekta ya Uchumi wa Buluu kupitia Utalii, Bandari, Mafuta na gesi pamoja na sekta ya usafirishaji wa majini.

Ameeleza kwa muda mrefu Zanzibar imekua ikitangaza Utalii wa zamani wa Urithi ukiwemo wa Mji Mkongwe wa Zanzibar na Fukwe, ameongeza kuwa wakati umefika Zanzibar sasa kuendelea kujitangaza pia na utalii wa kisasa ukiwemo utalii wa mikutano ya kimataifa, michezo, akitolea mfano michezo ya mbio za magari ambao umekua kivutio kikubwa duniani na kuwavutia mashabiki na wageni wengi maarufu kama (Formula one).

Aidha, Rais Dk. Mwinyi amesema dhamira ya Serikali ni kuwa na Utalii wa hadhi ya juu utakaowavutia wageni wengi kuja nchini bila kujali misimu ya utalii, pia amesema nchi imejiandaa kuwa na misimu yote ya Utalii kwa kuimarisha vivutio zaidi vyenye kuwavutia wageni wengi.

Kuhusu ongezeko la Utalii Dk. Mwinyi ameeleza dhamira ya Serikali kuendelea kuimarisha miundombinu ya barabara na mawasiliano ikiwemo viwanja vya ndege vya Unguja na Pemba kuemdelea kuwa na hadi ya kimataifa.

Akizungumzia masuala ya Uchumi na Uwekezaji Rais Dk. Mwinyi amesema Bado kuna maeneo mengi ya Uchumi ambayo wawekezaji wakija wanaweza kushirikiana na Serikali kuyaendeleza.

Kuhusu Bandari, Dk. Mwinyi amezizungumzia fursa za Bandari jumuishi kwa Zanzibar ambayo Serikali imewekeza nguvu kubwa huko Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja alikoeleza kwa sasa Zanzibar inahitaji Bandari kubwa ili kukidhi mahitaji ya uchumi wake kama kituo muhimu cha usafirishaji, usambazaji wa bidhaa, kutoa huduma na kufanyia biashara ikiwemo kupokelea mizigo, kusafirishia mazao, na mahitaji mbalimbali ikiwemo mafuta, nafaka, na kukuza uchumi wake.

Kwa upande mwengine Rais Dk. Mwinyi aligusia suala la mafuta na gesi pamoja na sekta ya usafirishaji wa majini, akieleza Zanzibar inavyohitaji uwekezaji mkubwa kwenye sekta hiyo na kuiomba Serikali ya Uengereza kuangalia uwezekano wa kuungamkono kwenye sekta hiyo kuimarisha sekta ya biashara na uchumi wa Zanzibar kupitia bandari zake za Uguja na Pemba.

Dk. Mwinyi pia aligusia eneo la nishati na kumueleza mgeni wake huyo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inadhamiria kuwa na umeme wa ukahkika kwa kuwa na umeme mbadala kwa ajili ya wawekezaji waliopo, hivyo, ameiomba Serikali ya Uingereza kuangaliua uwezekano wa kuweka nguvu zake kwenye eneo hilo.

Hata hivyo, Rais Dk. Mwinyi amewakaribisha wawekezaji zaidi wa Uingereza kuja Zanzibar kwa wingi kuwekeza na kunufaika na fursa za uwekezaji zilizopo.

Akizungumzia ukulima wa mwani, Dk. Mwinyi amemueleza balozi huyo kwamba Zanzibar inauza zao hilo kama malighafi kiasi ya kuwa halileti tija kwa Uchumi wa taifa na wakulima kwa ujumla, hivyo aliwashawishi wawekezaji kutoka Uingereza waje nchini waanzishe viwanda vya kuusarifu mwani na kuzalisha bidhaa za zao hilo jambo ambalo litawaongezea tija wakulima wa zao hilo nchini na bidhaa wanazozizalisha.

Pia amewaalika wawekazaji wa sekta binafsi wa Uingereza kuitembelea Zanzibar kubaini uzuri na fursa zilizopo.

Wakati huo huo, Rais Dk. Mwinyi ameishukuru Serikali ya Uingereza kwa ushirikiano wa diplomasia uliopo baina yao na Tanzania ikiwemo Zanzibar pia kwa kuisaidia Zanzibar kwa sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya na masuala mengine ya jamii.

Naye Balozi Marianne Young amemuhakikishia Rais Dk. Mwinyi kuwa Serikali ya Uingereza itaendelea kuunga mkono Zanzibar kuimarisha ustawi wa kuleta maendeleo hasa kwa masuala ya afya, elimu na Uchumi wa Buluu.

Amesema, Utalii ni fursa muhimu baina Zanzibar na Uingereza katika kuimarisha ushirikiano wa pande mbili hizo na kuiahidi Zanzibar kushirikiana kiufundi kwa uzoefu kwa masuala mbalimbali ya Uchumi, jamii na teknolojia.

Pia Balozi Young alisifu juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa maendeleo makubwa iliyofikiwa hasa kwa sekta ya mawasilino na miundombinu.

Alieleza Imani yake ya kuendeleza ushirikiano uliopo baina yao na kuahidi uuendeleza kwa vitendo na utekelezaji katika kuyafikia malengo baina ya pandembili hizo.

Balozi Marianne Young amechaguliwa wadhifa huo kuhudumu Tanzania mwezi Ogasti mwaka huu.

IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.

Related Posts