Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi, amesema Serikali inathamini mchango mkubwa wa wanasayansi, wahandisi, watafiti na wabunifu katika kufikia azma ya kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.
Prof. Mushi ametoa kauli hiyo leo Disemba 06, 2024 jijini Dar es Salaam akihutubia katika mahafali ya 18 ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) ambapo amewasisitiza Wahitimu kutumia kikamilifu elimu waliyoipata kwa maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla.
ββMafundi sanifu, wanasayansi na wahandisi ni nyenzo muhimu kwa nchi yetu kuchagiza maendeleo katika sekta mbalimbali za uzalishaji. Bila wataalamu hawa hatuwezi kustawi kiuchumiββ Alisema Prof. Mushi.
Katibu Mkuu huyo ameeleza kuwa Serikali imeendelea kuongeza fursa za mafunzo na kwamba katika mwaka wa fedha 2023/2024, iliongeza udahili katika Vyuo vya Elimu ya Ufundi kutoka wanafunzi 171,581 hadi wanafunzi 235,804.
Aidha imetoa mafunzo juu ya upimaji na ufundishaji wa mitaala inayozingatia umahiri kwa wakufunzi 843 wa Vyuo vya Elimu ya Ufundi, wakufunzi 45 kutoka katika vyuo hivyo wamepata mafunzo juu ya ufundishaji wa mitaala inayoendana na mabadiliko ya teknolojia na mahitaji ya soko la ajira.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi akizungumza katika mahafali ya 18 ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) ambayo yamefanyika leo Disemba 6, 2024 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi akikabidhi vyeti kwa wahitimu katika mahafali ya 18 ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) ambayo yamefanyika leo Disemba 6, 2024 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam