Boart Longyear yatoa msaada wa vifaa tiba kituo cha afya Lunguya wilayani Kahama

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Lunguya kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Msalala  mkoani Shinyanga, Dk.Yohana Msumba (kulia), akipokea Baiskeli kwa ajili ya kubebea wagonjwa kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Boart Longyear, Boniphace Mushongi wakati wa hafla fupi iliyofanyika mkoani humo juzi.

KAMPUNI ya Boart Longyear inayofanya kazi na mgodi wa Barrick Bulyanhulu katika kuadhimisha siku ya Ukimwi mwaka huu ilitoa Vifaa Mbalimbali katika Kituo cha Afya Lunguya Kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Msalala  Mkoani Shinyanga.

Akiongea baada ya kukabidhi vifaa hivyo Mtaalamu wa masuala ya afya wa kampuni hiyo Dkt. Alex Kamugisha, amesema wametumia maadhimisho haya mwaka huu kutoa msaada wa vifaa tiba na kushiriki kutoa elimu dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.

“Miongoni mwa vifaa tulivyotoa ni pamoja na seti ya televisheni ambayo itatumika Kuonyesha vipindi vya elimu ya afya lakini hapa ni sehemu inayopaswa kuwa katika mazingira ya usafi wakati wote tumeleta pia vifaa vya kufanyia usafi” ,alisema.

Kwa Upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho Dkt. Yohana Msumba Ameishukuru Kampuni ya Boart Longyear kwa kutoa Vifaa hivyo na kutambua Mchango wa kituo hicho katika Kuwahudumia wananchi.

Related Posts