Mbeya. Mwanaharakati na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mdude Nyagali aliyekuwa ameshikiliwa na Jeshi la Polisi, ameachiwa kwa dhamana.
Mdude alishikiliwa tangu Novemba 22 mkoani Songwe akiwa na viongozi wengine wa Chadema akiwamo Mwenyekiti wake Taifa, Freeman Mbowe na mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.
Baada ya kuhojiwa katika Kituo cha Polisi Songwe, kada huyo alipelekwa mkoani Mbeya kujibu tuhuma zinazomkabili ikiwamo matamko.
Wakili wa mwakanaharakati huyo, Philip Mwakilima amethibitisha kada huyo kuachiwa akieleza kuwa atafafanua zaidi atakapokuwa katika mazingira rafiki.
“Ni kweli ameachiwa naomba nitazungumza baadaye nikitoka mahakamani,” amesema wakili huyo kwa kifupi alipozungumza na Mwananchi Digital leo Desemba 6, 2024.
Endelea kufuatia mitandao ya Mwananchi