MAWADENI 147 WANOLEWA KUWAHUDUMIA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM

Na Mwandishi wetu- Dodoma

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Hamis Nderiananga amesema Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejenga na kukarabati miundombinu inayozingatia mahitaji maalum ya wanafunzi kuanzia elimu ya awali mpaka vyuo vikuu.

Mhe. Nderiananga aliyasema hayo mkoani Morogoro wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya kuwajengea uelewa Mawadeni 147 kutoka katika Taasisi za Elimu ya juu zinazopokea Wanafunzi wenye mahitaji Maalum.

Alieleza kwamba Serikali imeandaa na kusambaza miongozo ya Kitaifa ya utoaji wa elimu maalum na elimu jumuishi katika ngazi zote za elimu ikiwemo mwongozo wa shule ya nyumbani na mwongozo wa ubainishaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

“Serikali imenunua na usambazaji wa vifaa vya kielimu na teknolojia saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kuanzia elimu ya awali mpaka Elimu ya juu vikiwemo Laptops, Tablets, Digital Voice recorder, bajiji, shime sikio, viti mwendo, embosser machine na fimbo nyeupe, Obite Reader,”Alisema Naibu Waziri huyo.

Pia aliongeza kuwa Serikali imetoa ufadhili unaoitwa Samia Scholarship kwa wanafuzi wenye mahitaji maalum 32 waliofaulu kwa kiwango cha juu katika masomo ya Sayansi, Teknolojia na Hisabati kwa lengo la kuhamasisha usomaji wa masomo hayo na kuongeza fursa kwa wote.

Aidha Mkurugenzi wa Elimu Maalum kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Margret Matonya alibainisha kwamba Lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha kuwa Mawadeni wanapata stadi na maarifa ya namna ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili wanafunzi wenye mahitaji Maalum na kuwasaidia kutimiza ndoto zao.

Related Posts