Mwanasheria Mkuu wa Serikali Aahidi Kuboresha Sekta ya Sheria kwa Kutoa Dira kwa Wanasheria Nchini

Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari, ametoa ahadi ya kutoa mwelekeo kwa wanasheria wote nchini ili kuhakikisha wanatoa huduma za sheria serikalini kwa ufanisi, weledi, na ubora kwa kuzingatia mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa,teknolojia,tamaduni na hata kimazingira.

Ameyasema hayo hayo leo Desemba 6, 2024 Jijini Dodoma katika Kikao chake na wakurugenzi na Wakuu wa vitengo vya Sheria nchini ambapo wamekumbushana umuhimu wa kuzingatia sheria,taratibu,mipango ya maendeleo na miongozo mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Katika kikao hiki pamoja na mambo mengine kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali nitatoa Dira kwenye mambo ambayo tunadhani tunahitaji kuyazingatia katika Sekta ya Sheria nchini ili kuhakikisha wanasheria wote nchini wanatoa huduma za sheria serikalini kwa weledi na ubora kwa kuzingatia mabadiliko ya kiuchumi,kisiasa,teknolojia, tamaduni na hata kimazingira”. Amesema

Aidha Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameeleza kuwa lengo kubwa la Ofisi yake  kuwakutanisha Wanasheria hapo ni pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji katika utoaji wa huduma za kisheria kwenye taasisi za Umma ili kuboresha na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao.

“Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeandaa kikao hiki kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji katika utoaji wa huduma za kisheria kwenye taasisi za Umma ili kuboresha na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wetu katika Taasisi, Idara na Vitengo vya huduma za kisheria tunavyovisimamia”.

Naye Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe Samwel Maneno amelelzea suala la kutoa msaada wa kisheria kwa Wananchi ambapo amesema kuwa wao kama Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali tayari wanazo kliniki za utoaji wa huduma za kisheria kwenye Mikoa  yote kwaajimi ya kuhakikisha huduma hizi ambazo zimekusudiwa kutolewa na Ofisi hiyo zinatolewa ipasavyo na kliniki zinakuwepo mara kwa mara.

“Suala la kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi ni la moja kwa moja linaiguza ofisi yetu, na sisi tayari tunazo kliniki za utoaji huduma za kisheria kwenye mikoa yetu kwaaji ya kuhakikisha huduma hizi ambazo zimekusudiwa kutolewa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  zinatolewa ipasavya na kliniki zinakuwepi mara kwa mara”.

Kikao kazi hiki kimehudhuliwa na Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo vya Sheria takribani 300 kutoka Miko ya Tanzania Bara na Halmashauri zake.

Related Posts