NAIBU MRAJISI MKUU AMEVITAKA VYAMA VYA USHIRIKA KUJIKITA KATIKA MATUMIZI YA TEHAMA

 

Naibu Mrajis Udhibiti wa Vyama Vya Ushirika, Udhibitil, Collins Nyakunga mwenye mkasi wakishangilia mara baada ya kuzindua mfumo wa kieletroniki w huduma za kibenki wakati wa mkutano wa mwaka wa TRA Saccos iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Desmba 07, 2024.

Naibu Mrajis Udhibiti wa Vyama Vya Ushirika, Udhibitil, Collins akizungumza na waandidhi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba 07, 2024 mara baada ya kuzindua mfumo wa Kieletroni wa huduma za kibenki ambao upapatikana nchi zima


Naibu Mrajis Udhibiti wa Vyama Vya Ushirika, Udhibitil, Collins wapili kutoka kudhoto wakionesha kadi za umoja zitakazowasaidia kutoa pesa nchini.

Mwenyekiti wa TRA Saccos, Pili Marwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba 07, 2024 wakati wa Mkutano Mkuu wa TRA Saccos ambapo wamezindua Mfumo wa Kieletroni wa huduma za kibenki.

Mjumbe wa Bodi ya TRA SACCOS Ltd, Upendo Kunanga, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba 07, 2024 wakati wa Mkutano Mkuu wa TRA Saccos ambapo wamezindua Mfumo wa Kieletroni wa huduma za kibenki.

Mjumbe wa bodi ya TRA Saccos, Joel Lema akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba 07, 2024 wakati wa Mkutano Mkuu wa TRA Saccos ambapo wamezindua Mfumo wa Kieletroni wa huduma za kibenki.

Wanachama wa TRA Saccos wakiwa katika Mkutano mkuu unaofanyika leo na Kesho jijini Dar es Salaam.

NAIBU Mrajis wa Vyama vya Ushirika -Uthibiti, Collins Nyakunga amevitaka vyama vyote vya Ushirika kujikita katika matumizi ya teknolojia ya habari, Mawasiliano (TEHAMA) ili kutunza kumbukumbu na kurahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wanachama.

Nyakunga amesema hayo leo Desemba 7,2024 jijini Dar es Salaam wakati akimuwakilisha Mrajis Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania(TCDC)dkt. Benson Ndiege katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa TRA Saccos.

Sambamba na mkutano huo TRA Saccos pia wamezindua mtandao wa huduma za kibenki (TRA Mobile Application) na Pesa Kadi (ATM Card) itakayowezesha wanachama wake nchi nzima kutoa pesa kupitia benki ya CRDB, huku pia wakifanya uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2024.

Akizungumza katika mkutano huo, Nyakunga amewapongeza TRA Saccos kwa hatua hiyo walliyofikia na kusisitiza matumizi ya mfumo wa TEHAMA kwani dunia kwa sasa inakwenda kidigitali hivyo kumbukumbu nyingi zikiwa kwenye mfumo zitaweza kutunzwa vizuri na kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wanachama.

“Hivyo basi naelekeza wanachama kulipa malipo yao kwa kutumia mtandao na kupata mikopo bila shida yeyote na kufanya hivyo itasaidia kupunguza gharama na kukuza pato la chama,”Amesema

Ameiasa bodi itakayochaguliwa kuhakikisha inaendelea kukuza mtaji wa Chama kwa kuongeza kiwango cha hisa na akiba ya wanachama ili kuruhusu wanachama kugawana sehemu ya pato la Chama.

Aidha ameagiza elimu juu ya kujiunga na Ushirika kuendelea kutolewa kwa wafanyakazi wa TRA Kwani wengi wao wameoneka kutokuwa na elimu juu ya Ushirika huo na namna utakavyowasaidia hivyo elimu ikitolewa wanachama wataongezeka.

Pamoja na hilo Nyankunga amekitaka chama hicho kusajili mali zote za Ushirika ili ziweze kutambulika kwa mujibu wa sheria na pia amewalekeza wanachama kuendelea kuwekeza kwenye chama kwa kutoa fedha ili iuendelea kukuza mfuko na kuunga mkono wa jitihada za Rais Samia Suluhu.

Naye Mwenyekiti wa TRA Saccos,Pili Marwa alisema kupitia uzinduzi wa huduma za Kibenki kutasaidia wanachama hao kupata mkopo na kulipia huduma zote za kijamii bila shida kama vile kulipia maji,umeme na nyingine.

Amesema kupitia mfumo huo wataendelea kutoa mikopo hata kwa wale waliostaafu kwani bado wanasifa zote za uanachama na wamekuwa wakishiriki kwa namna moja ama nyingine kwa kutoa michango ya mawazo ya kuboreshaji wa Saccos hiyo.

Amesema Saccos hiyo mpaka sasa imeingia makubaliano na benki ya CRDB kuhudumia wanachama wao walio zaidi ya elfu 5000

Naye Mjumbe wa bodi kutoka TRA Saccos, Upendo Munanga alisema huduma iliyozinduliwa itaboresha zaidi maisha ya wafanyakazi wa TRA kwani pesa itapatikana muda wowote pale wanachama anapohitaji.

Naye Mjumbe wa bodi wa TRA Saccos,Joel Lema amesema mkutano huo umelenga kujadili maazimio ya Mkutano Mkuu uliopita na kupitisha bajeti ya mwaka huu itakayosaidia kuendesha chama.

Related Posts