SHIRIKA LA ACTIONAID TANZANIA LAJA NA MKAKATI KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA

Shirika lisilo la Kiserikali la Actionaid Tanzania kupitia Mradi wa TIF (Transformative Impact Fund) katika kuelekea maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia limeendesha kampeni yenye lengo la kutoa elimu kwa jamii kuendeleza kilimo kinachostahimili mabadiliko ya tabia nchi (Kilimo ikolojia) kwa wakulima wadogowadogo hasahasa wanawake na vijana.

Akizungumza na Wananchi mbalimbali Disemba 6,2024 wakati wa kampeni hiyo Katika Kijiji cha Mloda kata ya Mlowa Barabarani wilaya ya Chamwino Mwenyekiti wa Kijiji hicho Adam Philimon amewataka jamii kuachana na mila potofu yakuwa mtoto wakike hana haki ya kumiliki adhi kama mtoto wa kiume.

”Naupimaji huu maana yake ni utambuzi kwamba je tuangalie kuna ukatili kwa sababu hii hii ardhi siyo lazima umiliki we mwanaume, hii ardhi hakuna mtoto wa kike wa kunyimwa wote wanahaki hichi ndicho kilichokuwa kinafanyika ,”

”Serikali inavitu vingi vya kuweza kuangalia , lakini Mloda tumekuja kuona kwakweli umiliki wa ardhi tulivyoenda kuandikisha watu wengi wameandika watoto wao wakike na wakiume kwa jambo hili tunashukuru sana,”

Philimon amesema miongoni mwa ukatili uliokithiri katika kijiji hicho ni pamoja na wanaume kunyimwa ujumba na wake zao, watoto wa kike kuodheshwa katika umri mdogo ma kunyimwa haki zao za msingi ikiwemo kusoma.

“Wanaume wanaogopa tuu kusema hapa lakini matukio ambayo tumekuwa tukiyapokea hapa kijijini kwetu ni wanaume wengi kunyimwa unyumba na wake zao unakuta mtu anasema mwenyekiti mimi mke wangu kila nikihitaji ana nikatali.

” Na kunakesi moja make alikua hampi mume wake unyumba na haki hiyo anampatia mtu mwingine ambaye siyo Mume wake yaani ni kama anaishi na Mume Lakini unyumba anapewa MTU mwingine”amesema.

Aidha amesema matukio mengine wanaume kunyanyaswa na wake zao wenye vipato hasa mwisho wa mwaka ambapo akina mama wengi wanavunja vikoba vyao.

“Mwezi huu wa Disemba wakati akina mama wanavunja bikoba vyao tumekuwa tukipokea malalamiko mengi ya wanaume kunyanyaswa na wake zao Sisi kama serikali tunayapa sana malalamiko haya kutoka kwa wanaume wengi” Amesema.

Kwa upande wake Mratibu wa Shirika la Actionaid Tanzania Upande wa Mafia Samwel Mesiak amesema sababu inayochangia wanawake kutokumiliki ardhi ni pamoja na mila, destruri na imani potofu ambazo zilikuwepo toka enzi za mababu huku akiitaka jamii kuachana na imani hizo kwa kuwa kilimo ni nyezo ya uzalishaji katika jamii,”

”Mwaka huu tmekuja na kampeni yetu yakusema ya mwanamke kumiliki ardhi ni haki yake natupambane kikamilifu kuhakikisha tunafungua fursa za wanawake kumiliki ardhi, ukatili wa kijinsia haumaanishi tu kwamba kupiga mke, kumpiga mume, au kumnyima chakula lakini pia kwenye sekta ya uchumi,”

”Kuna mifumo ambayo ni kandamizi ambazo kwenye hizo sehemu tumepita tumekuja kugundua kwamba kikubwa ambacho kinamsamabisha mwanamke kutokumiliki ardhi wala siyo kwamba ni utashi kutokana na mila na desturi na tamaduni ambazo zimekuwepo enzi na enzi , sasa imefika muda mwafaka sasa wakuangalia kwamba nini kifanyike ili kumhakikisha huyu binti , mama, mdada kumiliki ardhi kama nyezo ya uzalishaji katika jamii,”

Akizungumza kwa niaba ya Wanawake wa Kijiji cha Mloda mhasibu wa Jukwaa LA Wakulima wanawake wadogo Wilaya ya Chamwino Nuru Mpanda ameendelea kuwahimiza wananchi na wakulima kwa ujumla kuwa mwanamke na mwanaume wote wananafasi ya kumiliki ardhi.

Naye Mratibu wa Mradi wa TIF (Transformative Impact Fund) kutoka Shirika la lisilo la kiserikali la Actionaid Tanzania Happy Itros amesema mradi huo unatekelezwa katika nchi nne ambazo ni Rwanda, Burundi, Tanzania na DRC , Kwa Tanzania upo Mikoa miwili Dodoma na Singida na Dodoma uko wilaya ya Chamwino katika vijiji kumi ambavyo ni Mlowa Barabarani, Mloda, Nzali, Kawawa, Msanga, Iringa Mvumi, Makang’wa, Chinangali II, Chamwino na Mahama.

Pia ameongeza kuwa lengo la mradi TIF ni kuwawezesha wakulima kupaza sauti za changamoto zao kwa kushiriki katika kutengeneza suluhisho kupitia majukwaa mbaimbali ya kijamii , pia kuchanganua sera na mipango mbalimbali zinazochangia kilimo ikolojia

Related Posts