Na Humphrey Shao, Michuzi Tv
Wasanii wa Muziki wa Bongo Fleva Chino Kid na kundi zima la Weusi usiku wa jana waongoza kwa kutoa burudani kwa wakazi wa Dar es salaam katika shoo kubwa waliyoifanya katika sherehe za Bata la Desemba zinazoendelea katika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaaam.
Katika shoo hiyo ya aina yake Chino kid aliweza kuwapagawisha watu alivyopanda na kundi lake zima la Wana Man Gang ambalo limeweza kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki waliofika uwanjani hapo kutokana na nyimbo zao na staili zao za kucheza za Amapiano mtindo ambao unapendwa na vijana waengi kwa sasa.
Mbali na Chino kid kuwasha moto katika bata hili lililoandaliwa na Bia ya Heinken Tanzania pia kundi zima la weusi linaloongozwa na Joh Makini liliweza kufanya sho kubwa ambayo aitosahaulika kwa wakazi wa Dar es salaam kutokana na staili yao ya kuingia jukwaani.
weusi ambao ilianza kuingia jukwaani kwa kuwakilishwa na G Nako ambaye alipanda na wacheza shoo wengi jambo ambalo ni nadra sana katika muziki wa Hip Pop hapa nchini jambo ambalo liliweza kuleta utofauti mkubwa na shoo zilizozoeleka.
Mbali na G Nako msanii mwengine wa Weusi aliyeweza kupanda ni pamoja na Lord Eye ambaye alivalia vazi la suti na staili yake ya kughani kwa mtindo wa taratibu huku akisikilizia biti linavyokwenda.