MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba ambaye kwa sasa anakipiga, Singida Black Stars, Habib Kyombo amejiunga na Pamba jiji kwa mkataba wa miezi sita.
Kyombo ambaye amepoteza namba kwenye kikosi cha kwanza cha Singida Black Stars anajiunga na timu hiyo kwa mkopo akitokea Black Stars.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo kimeliambia Mwanaspoti kuwa mazungumzo kwa pande zote mbili yamekamilika kinachosubiriwa ni dirisha la usajili kufunguliwa.
“Hatuna safu nzuri ya ushambuliaji tumecheza mechi 13 tumefunga mabao saba sio nzuri kwetu hivyo dirisha hili kocha katoa mapendekezo ya kuongeza nguvu eneo la ulinzi kiungo na ushambuliaji,” aalisema mtoa taarifa huyo na kuongeza;
“Hivyo maboresho bado yanaendelea kufanyia tunaamini hai dirisha linafunguliwa tutakuwa tumekamilisha usajili katika maeneo yote ambayo kocha ameomba yafayiwe kazi.”
Alisema vigezo wanavyozingatia kwenye kuboresha kikosi chao ni uzoefu kutokana na timu hiyo kujaza wachezaji wengi ambao ni vijana hivyo wanahitaji nguvu ya ziada ili waweze kuendana na kasi ya ushindani msimu wao wa kwanza kushiriki ligi.
Pamba Jiji ambayo imepanda daraja msimu huu inaendelea kujiimarisha ili kujiweka tayari kupambania nafasi ya kubaki ligi kuu msimu uajao tayari imeshakamilisha baadhi ya sajili ikiwa ni pamoja na mkongwe Kelvin Yondani, Deus Kaseke.