Accra. Rais wa zamani wa Ghana, John Mahama ambaye pia ndiye kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo, ameshinda tena urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana Jumamosi, Desemba 7, 2024.
Mahama aliwahi kuwa Rais wa nchi hiyo katika muhula wa mwaka 2012 hadi 2017.
Kiongozi huyo ambaye pia alikiwakilisha chama cha National Democratic Congress (NDC), amemshinda Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Mahamudu Bawumia aliyekuwa akikiwakilisha chama tawala cha New Patriotic Party (NPP).
Kabla ya tangazo hilo rasmi, Bawumia aliwaambia waandishi wa habari kwamba anaheshimu uamuzi wa Waghana kupiga kura kwa ajili ya mabadiliko. “Nimempigia simu Mheshimiwa John Mahama kumpongeza kama Rais mteule wa Jamhuri ya Ghana.”
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi