Utawala familia ya Rais Assad wa Syria uliodumu miaka 53 wadondoshwa

Utawala wa Rais Bashar al-Assad wa nchini Syria umeangushwa rasmi usiku wa kuamkia leo Jumapili, Desemba 8, 2024, baada ya waasi kuingia katika mji wa Damascus.

Taarifa zinasema Rais Assad na familia yake ambao wameitawala nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 53 wamekimbia kusikojulikana.

Picha za video zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zinaonyesha mamia wakivunja sanamu za familia ya Assad ziliopo mjini Damascus.

Milio ya risasi imesikika katika mji mkuu wa Damascus, wakati waasi nchini humo wakiendelea kupambana na vikosi vilivyokuwa vikimuunga mkono Rais Assad.

Rais Assad amekuwa Rais wa Syria tangu mwaka 2000 akipokea kijiti hicho kutoka kwa baba yake aliyefariki dunia Juni 10, 2000.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Related Posts