Wafanyakazi wa Ndani waomba kupewa mikataba ya ajira

Wafanyakazi wa ndani wameiomba Serikali kuhakikisha inaweka sheria maalum ya kuwabana waajiri wao ili waweze kupata Mikataba ya ajira.

Wakizungumza katika kongamano la kupinga Ukatili lilioloandaliwa na shirika lisilo la Seriali la Light For Domestic Workers (LDW) ambalo linajishughulisha na kutetea haki za wafanyakazi wa ndani baadhi ya wafanyakazi hao wamesema ukosefu wa Mikataba imekuwa changamoto kubwa sana katika utendaji wa kazi

Beatrice Johnson ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo la LWD anasema licha ya wafanyakazi hao kufanyakaz bila likizo kwa kipindi cha mwaka mzima lakini pia wanapita changamoto ya upatikanaji malipo Yao ya mishara pia imekuwa kikwazo kwao hali ambalo inasababisha wafanyakazi hao kukumbana na Ukatili wa kiuchumi.

Anasema changamoto nyingine inayowakumba wafanyakazi hao ni Ukatili wa kijinsia hasa kuitwa majina mabaya kama Beki tatu sambamsamba na kulazishishwa kufanya mapenzi kinguvu na wajiri wao au watoto wa waajiri.

Kwa upande wake polisi kata ya Chamwino Msafiri Hossein na amesema madhara ya kuwafanyia Ukatili wafanyakazi wa ndani wanarudisha vitendo hivyo Kwa watoto wanaowalea

Akizungumza katika hafla hiyo Maria Mapunda Mkurugenzi wa taaisisi ya mwanamke na Mafanikio ambaye alikua mgeni rasmi amesema suala la maslahi Kwa wafanyakazi wa ndani ni muhimu kwani ndio walezi wa watoto.

Anasema waajiri wanatakiwa kuishi kwa kuwapenda na kuwajali kwani ndio walezi wa watoto na familia kwa ujumla hiyo ni lazima wathaminiwe kama mwanafamilia .

Nao wakazi wa Mji wa Morogoro wamepongeza shirika hilo la LWD Kwa kutoa elimu kwa jamii kuwajali wafanyakazi wa ndani kwani ni kundi ambalo limesahaulika licha ya kuwa kiungo muhimu katika familia.

 

Related Posts