Mwaka 2024 unakwenda ukingoni, ukiangalia mshikemshike wa Ligi Kuu Bara umekuwa na mambo mengi. Katika kipindi cha mwaka mzima kuanzia Januari 2024 hadi Desemba 2024, timu 17 za ligi hiyo kati ya 18 zimefanya mabadiliko kwenye mabenchi yao ya ufundi. Makocha 22 wamefanyiwa mabadiliko.
Timu hizo 18 zinahusisha Mtibwa Sugar na Geita Gold ambazo zimeshuka daraja mwisho wa msimu uli-opita 2023-2024 sambamba na KenGold na Pamba Jiji zilizopanda daraja msimu huu 2024-2025. Mashujaa FC pekee ndiyo timu ambayo haijafanya mabadiliko hayo.
Ukiachana na rekodi hizo, ukiangalia msimu huu pekee ulioanza Agosti 2024 hadi sasa Desemba 2024 ikiwa ni takribani miezi minne, makocha 11 wameachana na timu walizokuwa wakizinoa.
Msimu uliopita 2023-2024, Singida Fountain Gate ambayo kwa sasa inatambulika kwa jina la Fountain Gate, ndiyo timu iliyoongoza kwa kufanya mabadiliko ya benchi lake la ufundi kuliko timu zote za Ligi Kuu Bara.
Ilianza na Mholanzi, Hans van Pluijim, kisha Mjerumani, Ernst Middendorp, akafuata Mbrazil Ricardo Heron Ferreira. Baada ya hapo ikawa zamu ya Msauzi, Thabo Senong, mwisho ikawa ni wazawa wawili Jamhuri Kihwelo na Ngawina Ngawina.
Katika msimu huo, ni makocha watano pekee walioanza na kumaliza wakiwa na timu zao ambao ni Youssoupha Dabo (Azam FC), Miguel Gamondi (Yanga), Abdulhamid Moallin (KMC) na Mohamed Abdallah ‘Bares’ (Mashujaa).
Kwa mwaka 2024 pekee, jumla ya makocha 22 wameachana na timu zao kwa sababu mbalimbali iki-wemo kumaliza mikataba, kupata dili sehemu nyingine lakini pia mwenendo wa timu kutokuwa mzuri nayo ni sababu nyingine ya kufanyika mabadiliko hayo.
Januari na Februari ilipita salama lakini ilipofika Machi, Tabora United ikatangaza kufikia makubaliano ya kuachana na Goran Kopunovic raia wa Serbia. Kocha huyo alitua kikosini hapo Agosti 2023.
Mwezi huo waliondoka makocha wawili. Kwanza alikuwa Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye alitambulish-wa ndani ya Singida Fountain Gate (kwa sasa Fountain Gate) Machi 2024 akipewa nafasi ya kuiongoza timu katika mechi 10 za mwisho, lakini hakukaa sana, kijiti kikaachwa kwa Ngawina Ngawina akamalizia msimu.
Baada ya Julio, ikafuata zamu ya Abdelhak Benchikha pale Simba SC ambapo Mualgeria huyu alitua Msimbazi Desemba 2023 kabla ya kuondoka Aprili 2024 akiwaachia Kombe la Muungano.
Ulikuwa ni mwezi wa kumaliza msimu wa Ligi Kuu Bara 2023-2024, hapa makocha sita vibarua vyao vilifi-ka ukingoni, wapo ambao mikataba ilimalizika kutokana na kukabidhiwa timu kukaimu nafasi ya kocha mkuu.
Juma Mgunda ambaye aliiongoza Simba akikaimu nafasi ya kocha mkuu, Abdelhak Benchikha ali-yeondoka Aprili, safari yake ndani ya timu hiyo ikaishia hapo. Mwingine ni Ngawina Ngawina ambaye alimaliza msimu akiwa anakaimu nafasi ya kocha mkuu pale Singida Fountain Gate.
Masoud Djuma naye msimu ulipomalizika akaachana na Tabora United, kumbuka kocha huyo raia wa Burundi, aliingia kikosini hapo Machi 2024 akiwa kocha msaidizi, kabla ya Mei kupewa mikoba ya kui-ongoza timu kama kocha mkuu.
Kocha Ahmad Ally naye akafikia ukomo katika kuiongoza Tanzania Prisons aliyokabidhiwa Novemba 2023, akatimkia JKT Tanzania alipo sasa.
Zuber Katwila aliyetua Mtibwa Sugar Oktoba 2023, safari yake kikosini hapo iliishia Mei 2024 ambapo mechi ya mwisho kuiongoza timu hiyo ilikuwa Mei 25, 2024 dhidi ya Mashujaa katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ugenini wakati timu ikiwa tayari imeshuka daraja huku ikibakiwa na mchezo mmoja kumaliza msimu.
Dennis Kitambi naye alifikia ukomo kuiongoza Geita Gold baada ya mchezo wa mwisho wa ligi uli-ochezwa Mei 28, 2024 nyumbani dhidi ya Azam huku timu hiyo ikiwa imeshuka daraja. Kocha huyo ali-tambulishwa hapo Desemba 20, 2023.
Mecky Maxime ambaye kwa sasa anaifundisha Dodoma Jiji, naye kibarua chake katika kikosi cha Ihefu ambayo hivi sasa inatambulika kwa jina la Singida Black Stars kilimalizika msimu ulipokwisha. Aliingia Desemba 2023.
Wakati msimu wa ligi 2023-2024 ukiwa umemalizika Mei, katika mwezi Juni klabu mbili zilitoa taarifa za kufikia makubaliano ya kuachana na makocha wake. Dodoma Jiji iliachana na Francis Baraza ambaye alijiunga na timu hiyo Desemba 2023, huku JKT Tanzania nayo ikifikia makubaliano ya kuachana na Malale Hamsini. Kocha huyo aliiongoza JKT Tanzania kwa msimu mzima.
Fred Felix Minziro aliyetua Kagera Sugar Januari 2024, aliondoka Agosti 2024 baada ya mkataba kumal-izika, pia Coastal Union ikaachana na David Ouma ambaye walimtambulisha Novemba 2023 akaiongoza timu kumaliza nafasi ya nne msimu wa 2023-2024 na kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika 2024-2025, wakaishia hatua ya awali.
Makocha wawili nao waliondoka mwezi huo. Wageni ndani ya Ligi Kuu Bara, KenGold, waliachana na Fikiri Elias, huku Azam nayo ikiachana na Youssouph Dabo aliyetua hapo Mei 2023.
Mwezi huu uliondoka na makocha wanne, kuna Francis Kimanzi aliyetambulishwa ndani ya Tabora United mwanzoni mwa msimu. Goran Kopunovic kwa mara nyingine tena baada ya mwanzo kuachana na Tabora United, safari hii ni zamu ya Pamba Jiji aliyojiunga nayo Julai 2024. Mwingine ni Paul Nkata ndani ya Kagera Sugar ambaye alitua hapo Agosti mwaka huu.
Mwinyi Zahera anahitimisha orodha hiyo baada ya Namungo kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi huku raia huyo wa DR Congo aliyetua kikosini hapo Desemba 2023 akipewa cheo cha mkurugenzi wa benchi la ufundi.
Unaweza kusema ni mwezi ambao ulitikisa kidogo kufuatia Yanga kutangaza kufikia makubaliano ya kuachana na Miguel Gamondi ambaye aliiongoza timu hiyo kubeba mataji mawili msimu uliopita am-bayo ni Ligi Kuu Bara na Kombe la FA huku pia akiifikisha timu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Kama haitoshi, msimu huu akaanza kwa kubeba Ngao ya Jamii akiifunga Simba nusu fainali kisha fainali akaichapa Azam. Kocha huyo ameondoka baada ya kuifikisha Yanga hatua ya makundi ya Ligi ya Ma-bingwa Afrika.
Wakati Gamondi anaondoka Yanga, klabu hiyo ikamchukua kocha wa KMC, Abdihamid Moallin ambaye amepewa cheo cha mkurugenzi wa ufundi.
Moallin aliiongoza KMC kwa msimu mzima wa 2023-2024 akimaliza nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi.
Mwezi ukakatika kwa Singida Black Stars kufikia makubaliano ya kuachana na Kocha Patrick Aussems ambaye alitambulishwa kikosini hapo Julai 2024. Aussems ameondoka Singida Black Stars akiiacha timu hiyo ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo ambapo aliiongoza katika mechi 10, alishinda 7, sare 2 na kupoteza moja mbele ya Yanga.
Akizungumzia timua timu ya makocha Ligi Kuu Bara, kocha wa zamani wa Mtibwa Sugar na Gwambina, Mohamed Badru anasema: “Sisi makocha kufukuzwa ni jambo la wakati wowote, lakini kwa mwenen-do huu tulionao sidhani kama ni sawa, nadhani klabu zinatakiwa kujitathimini kufukuza makocha hovyo sio tiba.”
Kwa upande wake, Patrick Aussems ambaye siku chache zilizopita aliondoka Singida Black Stars anase-ma: “Binafsi siamini kama niliondolewa kwa sababu ya mwenendo mbovu, tulishinda mechi saba, sare tatu na kupoteza moja, mpira wa Afrika huwa na mambo mengi nyuma, nadhani tunatakiwa kuhama huko na kufanya mambo kwa unyoofu katika kila eneo muhimu kwa ajili ya ukuaji wa soka letu.”