Meneja Biashara wa Kanda wa Airtel Tanzania, Faustin Mtui (kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya Router 50 za internet zilizotolewa na Airtel Tanzania kwa shule za sekondari wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro. Kulia ni Mtaalamu wa Vifaa na Muelimishaji kutoka Airtel Tanzania, Harrison Isdory. Msaada huo ni sehemu mradi wa Airtel Smartwasomi wa Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa lengo la kuhakikisha kila shule inatumia vifaa vya kidijitali kwa ajili ya kusomea na kufundishia.
Mtaalamu wa Vifaa na Muelimishaji kutoka Airtel Tanzania, Harrison Isdory, akizungumza na wananchi wa wilaya ya Rombo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Router 50 za intaneti zilizotolewa na Airtel Tanzania kwa shule za sekondari wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro. Msaada huo ni sehemu mradi wa Airtel Smartwasomi wa Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa lengo la kuhakikisha kila shule inatumia vifaa vya kidijitali kwa ajili ya kusomea na kufundishia.
Kaimu Afisa wa Elimu wa Wilaya ya Rombo, Adam Ally (Katikati) akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya Router 50 za internet zilizotolewa na Airtel Tanzania kwa shule za sekondari wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro. Wa pili kushoto ni Meneja Biashara wa Kanda wa Airtel Tanzania, Faustin Mtui. Msaada huo ni sehemu mradi wa Airtel Smartwasomi wa Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa lengo la kuhakikisha kila shule inatumia vifaa vya kidijitali kwa ajili ya kusomea na kufundishia.
Meneja Biashara wa Kanda wa Airtel Tanzania, Faustin Mtui (kushoto) akimkabidhi Mwalimu mkuu wa shule ya (insert name) katika hafla ya kupokea vifaa vya intaneti vitavyotumika shule za sekondari za wilaya ya Rombo, Kilimanjaro. Msaada huo ni sehemu mradi wa Airtel Smartwasomi wa Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa lengo la kuhakikisha kila shule inatumia vifaa vya kidijitali kwa ajili ya kusomea na kufundishia.
· Airtel yakabidhi vifaa vya Intaneti kwa shule 50 Kilimanjaro-Rombo
Kilimanjaro, – Airtel Tanzania imekabidhi vifaa vya intaneti (routers) 50 zitakazotumika kutoa huduma ya intaneti ya BURE kwa shule za serikali 50 wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya jitihada za Airtel Tanzania kuboresha mafunzo wa elimu kidijitali nchini Tanzania. Msaada wa vifaa hivyo ni sehemu ya mradi Airtel kwa kushikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto (UNICEF) uitwao Airtel SMARTWASOMI ambao umeundwa kwa lengo la kuziba ufa wa mgawanyiko wa kidijitali na kuziwezesha shule za serikali kupata nyenzo elimu za kujifunzia.
Akizungumza wakati wa makabidhiano, Meneja Biashara wa Airtel Mkoa Kilimanjaro, Faustin Mtui, aliipongeza serikali ya Tanzania kwa kuwekeza katika ushirikiano na sekta binafsi ili kuleta maendeleo ya sekta ya elimu.
“Vifaa hivi 50 vya intaneti (ODU) vitasaidia kuunga mkono jitiada za serikali za kutoa elimu ya kidijitali kwenye shule ya sekondari Rombo kwa kuwa vitawezesha upatikanaji wa nyenzo za kujisomea ambazo zinapatikana mtandaoni. Vifaa hivi vimeunganishwa na mradi wa Airtel Smartwasomi ambao utawapa walimu na wanafunzi mauddhui ya mtaondaoni BURE ambapo itawawafanya waende sambamba na maendeleo ya elimu kidijitali,” alisema Akyoo.
Kwa upande wake, kaimu Afisa Elimu wa Mkoa -Mwalimu Adam Ally alitoa shukrani za dhati kwa Airtel Tanzania kwa jitihada zake endelevu za kuimarisha sekta ya elimu nchini huku akisisitiza mchango muhimu wa ushirikiano katika kutatua changamoto za sekta ya elimu.
“Msaada huu utachangia kwa kiasi kikubwa maboresha ya mazingira ya kujifunza kwa wanafunzi ndani ya wilaya ya Rombo na kuhakikisha kuwa wanafanikiwa kitaaluma. Sanjari na hilo, walimu nao watapata nyenzo za kisasa za kufundishia, kutumia mbinu za kibunifu na kuboresha mafunzo yao na kuwafanya wafundishe kwa ufanisi zaidi,” alisema Mwalim Ally
Mradi wa Airtel Smartwasomi ulizinduliwa Mei 31, mwaka huu, kwa lengo la kuweka mifumo ya kidijitali ya kufundishia na kusomea kwenye shule za serikali takribani 3000 nchini Tanzania katika kipindi cha miaka mitano. Vifaa hivyo 50 ambavyo vitatolewa kwa shule za umma wilayani Rombo zitawawezesha wanafunzi kupata nyenzo za kujisomea, kuboresha uelewa wao na kuongeza ufaulu. Walimu pia watanufaika kwa kupata mbinu mpya za ufundishaji na rasilimali ili waweze kufundisha masomo yao kwa ufanisi zaidi.