DC MPOGOLO AONGOZA WAKAZI ILALA KUFANYA USAFI NA UPANDAJI MITI TISA DESEMBA

 

 Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ameungana na Watanzania bara katika kuadhimisha miaka 63 ya uhuru kwa kufanya usafi wa mazingira, na upandaji miti pembezoni mwa  fukwe ya habari ya Hindi. 

Zoezi la usafi lililoanzia katika soko la Ilala na buguruni limeshirikisha watendaji, wananchi na viongozi wa taasisi mbalimbali Mpogolo ameeleza dhamira ya Awamu ya sita katika kuhakikisha hali ya masoko inakua nzuri. 

Amesema Wilaya ya ilala imejipanga na iko tayari kuboresha mazingira ya biashara kwa kuboresha miumdombinu ya masoko kujengwa kisasa,  pamoja na kupata  kazi data kwa wafanyabiashara waliopo ili ujenzi unapokamilika waweze kurudi na kuondoa malalamiko ya baadhi yao kutopata nafasi. 

Akiwa katika fukwe za bahari ya hindi Mpogolo amebainisha mkakati wa kiweka taa katika barabara zote za jiji ili kusaidia kuongeza ulinzi kwa watumiaji wa maeneo hayo 

Aidha katika maadhimisho hayo, Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amewataka wakandarasi  wote kutekeleza wajibu wao kwa kufanya usafi wa mazingira pande zote za jiji la iala ili mji uwe safi. 

Akieleza  juu ya usafi wa jiji Mpogolo amewataka wafanyabiashara kurudi katika maeneo waliopangiwa ili kupisha matumizi sahihi za barabara ambazo kwa sasa wanapanga biashara zao. 

Huku akitoa angalizo kwa wanasiasa kutoingilia maamuzi ya kiutendaji katika kupanga jiji la ilala kwenye  usafi juu ya sheria na taratibu zinazotumika. 

Maadhimisho ambayo ilala  yameudhuriwa na Mkurugenzi wa jiji Elihuruma mabelya, Katibu tawala wilaya ilala Charangwa Suleiman, Kamishina msaidizi wa Jeshi la Magereza Gipson Mwakibibi, Nemc, Jeshi la Polisi, wananchi na viongozi wa kisiasa. 

Maadhimisho ya Miaka 63 ya Tanzania bara  yanaadhimishwa na kauli mbiu Uongozi madhubuti na ushirikishwaji wa wananchi ni msingi wa maendeleo.

Related Posts