LNa. Vero Ignatus, Arusha
Katika kuadhimiasha Miami 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana viongozi mbalimbali wa madhebu ya dini,wazee wa Kimila wamefanya maombi maalum kwaajili ya kuliombea Taifa.
Maombi hayo yamefanyika leo jumatatu 9 disemba 2024 Azimio la Arusha ambapo maelfu wamejitokeza kwenye matembezi ambayo yalianza majira ya saa mbili kamili asubuhi,kwenye mzunguko wa barabara ya Impala na kumalizikia kwenye mzunguko wa mnara wa Mwenge Jijini Arusha.
Akuzungumza Mkuu wa mkoa wa Arusha Christian Makonda amewataka wananchi wa Arusha kuhakikisha wanajiunganisha na Amani ya Taifa lao sambamba na uzalendo wa Taifa kwani lengo kuu la maombi hayo ni kuomba juu ya Taifa kutunza Amani kwani mkoa huo wameamua kumtanguliza Mungu na kumuabudu Mungu ili atambulikane katikati yao.
Amesema watu wengine wameamua kutengeneza madhabahu za kuwafarakanisha na Mungu hivyo wameamua kumtangaza ili watu waachane na miungu mingine”Arusha hatutaki Mambo ya kishirikina tunataka watu wote waende kwa Mungu “
“Tunajiuliza kwa nini mgeni anakuja Arusha anaona fursa anaichukua na anafanikiwa na wenyeji kubakia maskini jiulizeni kwa nini watoto wetu ni maskini, amueni kubadilika kwa kumuomba Mungu abadilishe mtizamo wetu alisema Makonda”
Leo Jumatatu wakati wa kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanzania bara, Mkoani Arusha kunafanyika matembezi na maombi maalum ya kuombea Mkoa wa Arusha kuanzia saa mbili kamili asubuhi, matembezi yakianzia kwenye mzunguko wa barabara ya Impala na kumalizikia kwenye mzunguko wa mnara wa Mwenge Jijini Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema Kuwa katika mkoa wa Arusha wameamua kumtanguliza Mungu na kumuabudu Mungu ili atambulikane katikati yao,watu wengine wameamua kutengeneza madhabahu za kuwafarakanisha na Mungu hivyo wameamua kumtangaza ili watu wamkimbilie “Arusha hatutaki Mambo ya kishirikina tu nataka watu wote waende kwa Mungu”
Kwa nini mgeni anakuja Arusha anyone fursa anaichukua na anafanikiwa na wenyeji kubakia maskini jiulizeni kwa nini watoto wetu ni maskini, kwa taarifa yenu Mungu hajawahi kupungukiwa kitu
Aidha amewaomba wananchi 24 disemba kila nyumba kuwe na kikao cha makakati na genda owe hivi tumekubali kuwa hivi hadi mwaka ujao au tunataka mabadiliko mtakachikubaliana muombeni Mungu awasaidie
Kwaupande wake Shekhe wa Mkoa wa Arusha Shaaban Bin Jumaa amesema Jambo linalifanyika Leo kwaajili ya NCHI yetu ndiyo tafsiri halisi ya uzalendo ni ishara ya kuonyesha upendo , hivyo kila mmoja amuombe Mungu ailinde Nchi ya Tanzania ili wananhi waweze kunufaika pamoja na vizazi vijavyo sambamba na kuilinda Amani iliyopo pamoja na Umoja uliopo.
” Kwenye Ubinadamu ndipo kwenye Umoja wa Taifa letu, viongozi wa mkoa wafanye Mambo kwaajili ya mkoa na Taifa la Tanzania,Kila zama Sina nyakati zinasema Mungu ayasimamie maono ya Mkuu wa mkoa kwani kila mwaka tumekuwa tulisheherekea Ila mwaka huu tumesheherekea kwa na hii
Naomba 24 disemba kila nyumba kuwe na kikao na genda owe hivi tumekubali kuwa hivi hadi mwaka ujao au tunataka mabadiliko mtakachikubaliana muombeni Mungu awasaidie
Kwa upande wake Nabii Mkuu Dkt Georgave amewatamkia Baraka wananchi wote waliokuwa katika maombi hayo kwamba kila neno baya lililotamkwa kwa mkazi wa Arusha limefutwa na kila manuizo yamefutwa na amewataka kwenda kufanikiwa na kunufaika.
Uhuru wa Tanganyika ulipatikana tarehe 9 Desemba 1961. Eneo la Tanganyika, ambalo awali, pamoja na Rwanda na Burundi, liliunda koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani, lilikuwa linasimamiwa na Uingereza kuanzia mwaka 1916 mpaka 1961. Kwanza lilikuwa linasimamiwa chini ya utawala wa kijeshi.