Mwenyekiti UWT Njombe atunukiwa Shahada ya Uzamivu

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Njombe, Scholastica Kevela ametunukiwa Shahada ya Uzamivu katika masuala ya fedha (PhD in Finance) na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Kevela ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Yono ametunukiwa PhD hiyo Desemba 5,2024 na Waziri Mkuu Mstaafu na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria, Mizengo Pinda, wakati wa mahafali ya 43 yaliyofanyika mkoani Kigoma.

Akizungumza Desemba 7,2024 wakati wa hafla ya kumpongeza Dk. Kevela amesema atatumia elimu aliyoipata kuhakikisha anawakomboa wanawake kiuchumi hasa walioko vijijini.

“Nimesoma PhD katika utu uzima, nimejifunza mengi na nimefanya utafiti wangu katika Mkoa wa Njombe kuangalia namna gani kinamama wa Mkoa wa Njombe watanufaika kiuchumi, kisiasa na kijamii kupitia taasisi za fedha, nimeangalia zinawasaidiaje kinamama wanaoongoza kaya vijijini.

Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Mizengo Pinda, akimtunuku Shahada ya Uzamivu katika masuala ya Fedha, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Njombe, Scholastica Kevela, wakati wa mahafali yaliyofanyika mkoani Kigoma.

“Tungetamani kupitia ‘microfinance institution’ kinamama wawezeshwe kunufaika kiuchumi, mama awe na uwezo wa kumiliki nyumba, kusomesha watoto, ninachowaambia Watanzania hakuna kukata tamaa, watoto wetu, wanawake tunatakiwa tukaze buti,” amesema Dk. Kevela.

Ameishauri Serikali kuzitupia macho taasisi za fedha hasa zile zilizoko vijijini ambako ndiko kuna Watanzania wengi kwa kuhakikisha wanaongeza mitaji ili waweze kukopa mikopo mikubwa itakayowafaa maishani mwao.

Dk. Kevela pia amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi bora na kwa kuweka mazingira mazuri ya elimu ambayo yamewasaidia Watanzania wengi kujiendeleza kielimu.

“Tunamtazama Dk. Samia Suluhu kama ‘Roll model’ wetu, niwahamasishe vijana wa Tanzania na kinamama wenzangu twende darasani, elimu inasaidia kukuza uelewa. Chuo Kikuu Huria ni rafiki, unaweza kusoma ukiwa unaendelea na majukumu mengine,” amesema Dk. Kevela.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema Watanzania wanayo matumaini makubwa kwa wahitimu wa ngazi mbalimbali katika chuo hicho kwa kuwa ndiyo chachu katika maendeleo ya nchi.

Mahafali hayo yamehusisha wahitimu 4,307 na kati yao 55 w

Related Posts