Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo DCP Kombo Khamis Kombo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.
Kombo anachukua nafasi ya CP Hamad Khamis Hamad aliyeteuliwa kuwa Balozi.
Pia, amempandisha cheo DCP Tatu Jumbe kuwa Kamishna wa Polisi na kuteuliwa kuwa Kamishna wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu katika Jeshi la Polisi.
Tatu anachukua nafasi ya CP Suzan Kaganda aliyeteuliwa kuwa Balozi.
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Jumatatu, Desemba 9, 2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Sharifa Nyanga.