KOCHA wa zamani wa Simba, Abelhak Benchikha ametaja makosa matatu ambayo Simba na Yanga zinapaswa kuyafanyia kazi kwa haraka kama wanataka kutoboa kimataifa.
“Kosa la kwanza; Zinapoteza mpira kirahisi na unapocheza na timu kubwa huo ni mtaji mkubwa kwa wapinzani, kwani wao huwa wanatumia kila kosa kama fursa.
La pili:”Safu zao za ulinzi nazo zilifanya makosa makubwa ya kiulinzi ndiyo maana kila walipoacha nafasi moja goli liliingia, Hivyo safu inatakiwa icheze kwa nidhamu kubwa, timu zote zilifanya kosa hilo na zikaruhusu mabao mawili ya haraka.
Mwisho ni safu zao za ushambuliaji, Kwa Yanga wakati nikiwa Simba nilikuwa naihofia sana kwa sababu kila mchezaji alikuwa na uwezo wa kufunga kitu ambacho kimepungua sasa.”
Aliongeza:”Yanga safu yake haitengenezi nafasi za kutosha pia na Simba lakini siwezi kuwalaumu washambuliaji wa Wekundu sababu timu yao haikutengeneza nafasi nyingi za kufunga.”
“Lakini bado timu zote zina nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi zilizosalia, wanachotakiwa kutambua ni wanakwenda kucheza mechi kubwa wanatakiwa wajiandae kwa ukubwa.”