Kesi ya Netanyahu inahusu mashtaka ya aina gani? – DW – 10.12.2024

Kimsingi kiongozi huyo anakabiliwa na mashtaka gani? Netanyahu alishtakiwa mwaka 2019 kwa tuhuma za hongo, ulaghai na kukiuka uaminifu, yote ambayo Netanyahu anayakanusha. Kesi yake ilianza 2020 na inahusisha kesi tatu za jinai. Anakanusha mashtaka na amekana kuwa na hatia.

Katika kesi namba 4000, Waendesha mashtaka wanadai Netanyahu alitoa upendeleo wa kandarasi yenye thamani ya kama dola milioni 500 kwa kampuni ya mawasiliano ya Israel -Telecom Israel, wakisema yeye na mkewe Sara wakisaka kupewe nafasi ya upendeleo wa kuandikwa vizuri katika tovuti ya habari ambayo inayodhibitwa na mwenyekiti wa zamani wa kampuni hiyo, Shauil Elovitc.

Katika kesi hii, Netanyahu ameshtakiwa kwa hongo, ulaghai na kuvunja uaminifu. Katika kesi nyingine namba 1000 kiongozi huyo ameshtakiwa kwa kufanya kwa kuvunja uaminifu kufuatia tuhuma kwamba yeye na mkewe walipokea kimakosa kiasi cha dola laki mbili na kumi kama zawadi kutoka kwa mtengeneza filamu wa Hollywood, Musrael Arnon Milchan na bilionea wa Australia James Packer.

Waendesha mashitaka walisema zawadi ilijumuisha champagne na sigara na kwamba Netanyahu alimsaidia Milchan katika maslahi yake ya kibiashara. Packer na Milchan hawakushtakiwa.

Kesi nyingine namba 2000, Netanyahu anadaiwa kufanya mazungumzo na Arnon Mozes, mmiliki wa gazeti la Israel la Yedioth Ahronoth, ili apate nafasi ya kutangazwa vyema katika chombo chake kwa malipo ya kuwepo kwa kanuni za kumpungiza nguvu upinzani wa kibaisahra dhidi yake. Netanyahu ameshtakiwa kwa udanganyifu na uvunjaji wa sheria uaminifu.

Uamuzi utatolewa lini kuhusu kesi zinazomkabili Netanyahu?

Israel| Netanyahu
Vita kati ya Israel na kundi la Hamas vilipunguza mbinyo wa kisiasa na kisheria ulikuwa unamkabili Benjamin Netanyahu. Picha: Kobi Gideon/Israel Gpo via ZUMA Press Wire/picture alliance

Hoja nyingine kesi zote hizi uamuzi wake utatolewa lini? Na uchambuzi unaonesha kuwa atachukua muda mwingi kabla ya majaji kutoa uamuzi.

Hoja nyingine kwa namna gani Netanyahu ataendelea kuwa katika kizimba cha mahakama huku akisalia kuwa bado waziri mkuu? Sheria za Israel zinasema kwa waziri mkuu hakuna ulazima wa kujizulu mapaka pale atakapokutwa na hatia. Na hata kama akikata rufaa ataendelea kuwa madarakani katika kipindi chote cha rufaa yake.

Hukumu kwa kesi ya rushwa ni kufungo cha hadi miaka 10 gerezani au faini. Lakini Ulaghai na uvunjaji wa uaminifu huadhibiwa hadi miaka mitatu gerezani.

Shambulio la Hamas kwa Israeli la Oktoba 7, 2023, na kufuatiwa kwa vita vya Gaza, vilififisha nguvu katika kesha ya Netanyahu ambapo Waisraeli walikusanyika kwa huzuni na kiwewe. Kabla ya vita, matatizo ya kisheria ya Netanyahu yaliwagawanya sana Waisraeli na kutikisika siasa za Israel.

Baada ya ushindi wa Netanyahu wa 2022 kwenye sanduku la kura, serikali yake ya mrengo mkali wa kulia ilianzisha kampeni ya kisheria ili kupunguza mamlaka ya mahakama. Ilizua maandamano makubwa nchini Israel na hofu miongoni mwa washirika wa Magharibi kwa ustawi wa kidemokrasia kwa Israel.

Related Posts