Samia amtaka Profesa Janabi kujiandaa kumrithi Dk Ndugulile WHO

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi kujiandaa kugombea nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Dk Faustine Ndugulile.

Dk Ndugulile ambaye pia alikuwa Mbunge wa Kigamboni, alifariki dunia Novemba 27, 2024 ikiwa ni miezi kadhaa baada ya kushinda nafasi hiyo.

Akizungumza mara baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali leo Jumanne, Desemba 10, 2024 kwenye Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar, Rais Samia amesema wamepitia wasifu zaidi ya 500 na kubaini kwamba, Profesa Janabi ana sifa ya kurithi mikoba hiyo.

“Naomba nifichue siri hapa, tumepitia zaidi ya CV tano na tukaona Profesa Janabi anafaa kuchukua nafasi ya Dk Ndugulile. Hivyo, tunakundaa kwenda kugombea nafasi hiyo muda utakapofikia. Ujiandae,” amesema Rais Samia

Dk Ndugulile alitarajiwa kuanza kazi rasmi WHO Machi 2025, baada ya kupewa miezi sita ya kujipanga.

Dk Ndugulile alikuwa Mtanzania wa kwanza, pia wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kushika nafasi hiyo.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Related Posts