Timu za taifa pekee kushiriki Mapinduzi Cup 2025 ,Simba na Yanga kukosekana

Kamati ya mashindano ya kombe la Mapinduzi kupitia Makamo Mwenyekiti wake ndugu Suleiman Jabir rasmi yatoa muongozo wa mashindano hayo

Mfumo wa mashindano hayo msimu huu 2025 utajumuisha timu za taifa badala ya timu za vilabu hii ni kufuatia Tanzania , Kenya na Uganda kuwa wenyeji wa mashindano ya Afcon na CHAN ili kutoa fursa ya kupata mazoezi kwa timu za Taifa .

Mashindano yanatarajiwa kuanza tarehe 3 January2025 na fainali kuchezwa Tarehe 13 January 2025

kabla ya hapo kutakua na droo maalum yakupanga makundi ya mashindano hayo na mashindani hayo kwa msimu huu yatafanyika katika uwanja wa Gombani Pemba baada ya uwanja wa Amaan kuwa katika maboresho

Timu za taifa ambazo zitashiriki ni pamoja na Zanzibar Heroes , Kenya , Uganda , Kilimanjaro Stars , Burundi na Burkinafaso .

Bingwa atapata milion 100

Related Posts