Mkuu wa biashara wa Haier Tanzania, Ibrahim Kiongozi akibadilisha mkataba na Mkuu wa Kitengo cha biashara Airtel Tanzania, Caroline Lyimo wakati wa hafla ya kuingia mashirikiano kati ya Haier na Airtel, Tukio la ushirikiano huo limefanyika katika hoteli ya King Jada jijini Dar es Salaam leo, Desemba 10, 2024.
KAMPUNI ya Airtel imeingia mashirikiano ya Kimkakati na GSM Haier Tanzania ili kuboresha huduma ya intaneti kwa Watanzania, Kupitia ushirikiano huo wateja watakaonunua runinga za Haier zenye ukubwa wa kuanzia inchi 50 hadi inchi 98 watapata Router ya 5G bure pamoja na kifurushi cha intaneti cha mwezi mmoja bure.
Ushirikiano huo unalenga kuwapatia Watanzania muunganisho wa intaneti usio na kikomo na chaguo bora la burudani, hivyo kuboresha maisha ya kisasa na urahisi majumbani.
Ushirikiano huo unaonesha dira ya pamoja ya kampuni zote mbili ya kuleta suluhisho bunifu nafuu na la kuaminika kwenye soko la Tanzania. Kwa kuunganisha utaalamu wa Haier katika teknolojia ya nyumbani mahiri na huduma za muunganisho za Airtel, ushirikiano huu unajibu mahitaji yanayoongezeka ya teknolojia ya kisasa na muunganisho wa kuaminika nyumbani.
Akizungumza katika hoteli ya King Jada jijini Dar es Salaam leo Desemba 10, 2024 kuhusu ushirikiano huo Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel Tanzania, Joseph Muhere, ameeleze ushirikiano wa kampuni hizo mbili na jinsi utabadilisha maisha ya kisasa katika familia za Tanzania.
“Tunawapa wateja wetu fursa ya kufurahia urahisi na maisha ya kisasa kwa kuunganisha mtandao wetu wa kasi na wa kuaminika na vifaa bunifu vya Haier, pia unakamilisha lengo letu la kurahisisha maisha ya wateja wetu kupitia suluhisho na bidhaa za kidijitali za hali ya juu.” Ameleza Muhere.
Kwa upande wa Mkuu wa Biashara wa Haier Tanzania, lbrahim Kiongozi, ameonyesha kufurahishwa na ushirikiano huo.
“Haier imejikita katika kuboresha maisha ya Watanzania kupitia teknolojia bunifu na rahisi inayopatikana. Ushirikiano wetu na Airtel Tanzania ni uthibitisho wa dhamira hi, kwa kuunganisha nguvu za chapa mbili zinazoongoza ili kuwapatia Wateja uzoefu Na kipekee wa kisasa.” Amesema Kiongozi
Ameeleza kuwa Kampeni hiyo inapatikana katika maduka teule ya chapa ya Haier nchini Tanzania, ikiwemo Samora Posta, Mlimani City, na Uhuru Street jjini Dar es Salaam, pamoja na Rock City Mall
jijini Mwanza.
Hafla hiyo ilihusisha maonyesho ya moja kwa moja ya kifaa cha Airtel 5G Router na runinga mahiri za Haier zikifanya kazi kwa pamoja, zikionesha jinsi teknolojia hizi mbili zinavyoshirikiana kutoa uzoefu mpya na bora wa burudani nyumbani.
Mpango huu unatarajwa kufanya teknolojia ya kisasa kupatikana kwa urahisi zaidi huku ukijibu mahitaji yanayoongezeka ya muunganisho wa kuaminika nyumbani nchini.