WATUMISHI wa Tume ya Ushindani (FCC) wameanza mafunzo ya Kuchakata Takwimu kwa kutumia Excel katika Chuo cha Takwimu lengo likiwa kuwajengea uwezo katika kurahisisha uchakataji wa takwimu.Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu ambae pia ni Mkurugenzi wa Tafiti, Miungano ya Makampuni na Utoaji kutoka FCC Bi. Zaytun Kikula amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa kwa tume katika kuimarisha ufanisi wa kazi kwenye maeneo tofauti, pia mafunzo haya yanahusisha watumishi 25 kutoka vitengo mbalimbali vya tume.
Ameishukuru menijimenti ya Tume hiyo kuona umuhimu wa kutoa mafunzo na elimu kwa watumishi wake na kusisitiza mafunzo hayo yanakwenda kuboresha utendaji kazi kwa watumishi pamoja na kuogeza kasi ya ufanisi katika sekta mbalimbali za FCC
“Tunamshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwani amekuwa akihamasisha sana watumishi wapewe mafunzo ili kuleta tija na faida katika taifa letu.Niwaombe watumishi wa FCC kutumia vizuri mafunzo mtakayoyapata yalete tija kwa taifa letu na elimu hii mkawape na wengine ambao hawajaipata.”
Awali Makamu Mkuu wa Chuo Mipango,Fedha na Utawala Dkt. France Shayo akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo amesema watumishi hao 25 watakapomaliza watafanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.
“Tunaishuru Menejimenti ya FCC kuwaleta watumishi wao kujifunza katika chao chetu na sisi tutawapa elimu ya kutosha namna ya kutumia Excell kwenye kuchakata data. Pia nitoe rai kwa wakuu wa taasisi mbalimbali kuleta watumishi wao kuja kujifunza kama walivyofanya watumishi wa FCC”
Kwa upende wake Meneja wa Kumlinda Mlaji Tume ya Ushindani (FCC),Bw. Joshua Msoma
ameushukuru uongozi wa tume na uongozi wa chou cha takwimu na anaamini watumishi hao watakapokamilisha mafunzo hayo yatawasaidia wakiwa wanatekeleza majukumu yao mbalimbali.