Na Malima Lubasha, Serengeti
WAZAZI na Walezi wa wanafunzi wanaosoma Shule ya Msingi Mapinduzi, Kata ya Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara,wametakiwa kuwalinda watoto wao na kuacha kuwapa kazi ya kufanya biashara wakati wenzao wanaendelea na masomo.
Ushauri huo umetolewa na Polisi Kata ya Mugumu, Mkaguzi Msaidisi wa Polisi, Pius Kahabi wakati alipozungumza na wazazi,walezi na walimu wa shule hiyo katika mkutano ulioitishwa na uongozi wa shule ili kupokea taarifa ya maendeleo,matokeo ya mtihani na changamoto mbalimbali zinazokabiri shule hiyo.
Kahabi amesema kuwa wakati akiwa anasimamia dawati la jinsia wanawake na watoto pale polisi kabla ya kuteuliwa kuwa polisi kata hiyo alikamata watoto wakizurura mjini wengine wakifanya biashara huku wengine wakiwa shule wanasoma ambapo walipohojiwa walidai kazi hizo wameagizwa na wazazi kutafuta pesa za matumizi nyumbani.
Amesema kuwa watoto hao kufanya biashara ndogo ndogo mitaani na kushindwa kuhudhuria masomo wamekosa uangalizi kutoka kwa wazazi na walezi ambao ndio walinzi wakisaidiwa walimu kulea jambo hili halikubariki hivyo watoto watakaokamatwa na kufikishwa polisi watashughulika na wazazi ambao hawachukui hatua kwa watoto wao.
Pia Mkaguzi Msaidizi huyo wa Polisi amesema kutokana na wazazi kushindwa kufuatilia maendeleo ya watoto wao kama wanahudhuria shule kila siku imebainika kuwa wanafunzi wengi wamekamatwa waki cheza michezo ya kubahatisha wakiwa na sare za shule wakitumia pesa ambazo wanapata wapi bila mzazi kujua.
“ Itafanyika oparesheni maalum ya kukamata watoto wanaocheza mchezo huo na kuacha kwenda shule badala yake hatua itachukuliwa mzazi kwani PS hairuhusu watoto waliochini ya umri wa miaka 18 kuche za na wamiliki wa PS hizo wasiruhusu watoto wa aina hiyo kucheza,”amesma Kahabi.
Kahabi amesema kuwa wazazi wanao wajibu wa kuhakikisha watoto wao wa kike na kiume wanapata ha ki yao ya elimu kwani sheria namba 21 ya mtoto inaeleza mtoto ni yule aliye chini ya umri wa miaka 18 apate haki yake ya kupata elimu bora.
Naye Mratibu Elimu Kata ya Mugumu,Sofia Chamriho,amesema kuwa changamoto hiyo ya watoto kuach akuhudhuria shule na kwenda kufanya biashara wakati wa masomo ipo na kueleza kwamba hali hiyo ina tokana na mifarakano ya ndoa inayoathiri watoto.
Pia Chamriho ameonya na kuwataka wazazi na walezi kusimamia suala la elimu kwa watoto wao kuwaa chia kujiende sha wenyewe hali ambayo inachangia kujiingiza katika vitendo vibaya vya utoro wa reja reja na biashara kwa wanafunzi na kusisitiza wazazi kuchangia umuhimu wa wanafunzi kupata chakula shuleni lengo ni kusaidia kuongeza ufaulu katika masomo na mtihani.