Yas Tanzania yashinda tuzo – Mtanzania

Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya Mawasiliano ya @yastanzania_ imeshinda Tuzo ya kuwa kampuni namba moja ya Mawasiliano yenye mtandao wa Internet wenye kasi zaidi “OOKLA SPEEDTEST AWARD FOR THE FASTEST MOBILE NETWORK IN TANZANIA” ambapo kampuni ya YAS imeibuka mshindi wa kwanza kwa mwaka 2024 nakuziacha mbali kampuni zingine zinazotoa huduma ya mawasiliano nchini

Akitangaza ushindi huo wa YAS TANZANIA hii leo Jijini Dar es Salaam, Kaimu CEO wa kampuni ya YAS Tanzania, Jerome Albou amesema wamekuwa washindi wa tuzo hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo na kwamba Yas Tanzania imepiga hatua kubwa kwenye kutoa huduma ya Internet yenye kasi zaidi nchini hivyo kukidhi vigezo vya kitaifa.

Aidha Albou amesema kampuni hiyo imewekeza jumla ya Trilioni 1 za kitanzania katika kuhakikisha Tanzania Bara na Visiwani inakuwa na minara 4000 ya kiwango cha 4G huku wakiifikidha 5G kwenye miji yote mikubwa Tanzania

“YAS Tanzania imedhamiria kubadilisha sekta ya Mawasiliano kwakuwapa wateja wake huduma zakisasa za Kiteknolojia zinazohitajika sokoni kwalengo la kukuza biashara, kuleta usawa na upatikanaji wa huduma jumuishi, ubunifu katika Teknolojia na hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi” Amesema.

Ameongeza kuwa wanapo sherehekea ushindi huu wa Tuzo kutoka OKLA bado wanazingatia jukumu lao la kutoa huduma bora katika sekta ya Teknolojia ya Mawasiliano nchini, na kwamba wamejiwekea malengo madhubuti ya kuongeza wigo wa upatikanaji wa mtandao imara na kuleta mapinduzi katika sekta ya kidigitali

Akizungumzia ushindi wa tuzo hiyo, Osama Nawayse kutoka Ookla amesema, kampuni ya hiyo imeshinda kwa asilimia 68.81 kwa kuwa na Internet yenye kasi zaidi na hakuna kampuni yoyoye ya mawasiliano Tanzania imefikia kiwango hicho.

Kwa upande wa Medium dowloder speed YAS TANZANIA imepata asilimia 43 ikizitangulia kampuni zote za mawasiliano nchini Tanzania sambamba na kuongoza katika vipengele vingine tofauti tofauti kuhusiana na masuala ya upatikanaji wa Internet yenye kasi zaidi nchini Tanzania.

Related Posts